IQNA

Waislamu 20 wauawa katika hujuma ya kigaidi nchini Ethiopia

15:34 - April 28, 2022
Habari ID: 3475181
TEHRAN (IQNA)- Genge moja la magaidi wa Kikristo lililokuwa limejizatiti kwa silaha nzito limewavamia na kuwaua Waislamu zaidi ya 20 katika mji wa Gondar wa kaskazini mwa Ethioia wakati Waislamu wao walipokuwa kwenye maziko ya mzee mmoja wa Kiislamu.

Baraza la Masuala ya Kiislamu la Amhara ambako ndiko uliko mji huo wa Gondar limesema kuwa mauaji hayo yaliyofanywa na genge hilo la Kikristo lenye misimamo mikali, ni mauaji ya umati dhidi ya Waislamu. Genge hilo la Kikristo limewafyatulia risasi kiholela Waislamu kwa kutumia silaha nzito na maguruneti na kuua idadi kubwa ya Waislamu hao na kujeruhi wengine wengi ambao hivi sasa wamelazwa hospitalini. Baraza hilo la Masuala ya Kiislamu la jimbo la Amhara huko Ethiopia lilithibitisha jana Jumatano kuwa zaidi ya Waislamu 20 wameuliwa kigaidi katika shambulio la genge hilo la Kikristo ambalo kimsingi lililotekea siku ya Jumanne. Magaidi hao walipora pia mali za Waislamu kwenye jinai hiyo.

Meya wa mji wa Gondar, Zewdu Malede ameliambia Shirika la Utangazaji la Ethiopia (EBC) kwamba jinai hiyo imefanywa na watu wenye misimamo mikali, lakini hakutoa ufafanuzi zaidi kuhusu ni genge lipi la Wakristo lililofanya jinai hiyo.

Mashirika ya Magharibi yanadai kuwa Waislamu wanaunda thuluthi ya wananchi milioni 110 wa Ethiopia. Idadi yao katika jimbo la Amhara ni ndogo ingawa jimbo hilo ni la pili kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wakazi nchini humo. Wakristo wa kanisa la Orthodox ndio wanaolidhibiti kikamilifu jimbo la Amhara la kaskazini mwa Ethiopia. 

Mwaka 2019 Misikiti kadhaa ya Waislamu ilishambuliwa katika mji wa Mota wa jimbo hilo la Amhara ambalo liko umbali wa zaidi ya kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu Addis Ababa. Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed alilaani vikali jinai hiyo iliyofanywa na Wakristo dhidi ya Waislamu. 

3478691

Kishikizo: waislamu ethiopia Amhara
captcha