IQNA

Njama za Wazayuni dhidi ya al Quds
16:15 - May 24, 2022
Habari ID: 3475289
TEHRAN (IQNA) - Taasisi kadhaa za Kiislamu mjini al-Quds (Jerusalem) zimeonya dhidi ya kuzuka kwa vita vya kidini kama uamuzi wa mahakama ya Israel ambao unaruhusu Wayahudi kufanya ibada ndani ya eneo la Msikiti wa Al-Aqsa.

Baraza la Wakfu, Masuala ya Kiislamu na Maeneo Matakatifu; Idara ya Wakfu za Kiislamu; Tume Kuu ya Kiislamu; Taasisi ya Fatwa ya Palestina; na Mahakama ya Jaji Mkuu wa Al Quds (Jerusalem) zote zinapinga uamuzi wa Mahakama ya Mahakimu wa Israel mjini Quds mbayo iliwaidhinisha Wayahudi kufanya matambiko yao ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa.

"Hatutambui uamuzi wowote unaohusiana na Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa uliotolewa au kupitishwa na mahakama yoyote au upande wowote," walisema Jumatatu.

Taarifa hiyo ya pamoja ilikariri kuwa chombo pekee kinachohusika na mipango ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa ni Idara ya Wakfu za Kiislamu, na kwamba kazi inasimamiwa na serikali Jordan ambayo ina mamlaka ya usimamizi wa maeneo matakatifu katika mji huo mtakatifu. "Maamuzi yote kama haya yanayolenga kuuyahudisha Msikiti wa Al-Aqsa ni batili."

Taasisi hizo za kiislamu pia zimefichua kwamba uvamizi wa Israel umeugeuza Msikiti wa Al-Aqsa kuwa "kambi ya kijeshi" ili kusimamia mashambulizi ya kila siku ya walowezi wa Kiyahudi wenye itikadi kali, na kuonya kwamba hali hii inaweza kusababisha "vita vya hatari vya kidini."

Walionya utawala vamizi wa Israeli kwamba lazima ubebe dhima ya matokeo ya uwepo mkubwa wa kijeshi katika Msikiti wa Al Aqsa na uvamizi wa kila siku wa walowezi wa Kiyahudi katika eneo hilo.

3479042

Kishikizo: aqsa ، palestina ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: