IQNA

Jinai za Wazayuni

Israel yaonywa kuhusu kufanya mabadiliko yoyote katika Msikiti wa Aqsa

16:58 - July 02, 2022
Habari ID: 3475451
TEHRAN (IQNA)- Mabadiliko yoyote ambayo utawala haramu wa Israel unapanga kutekeleza katika hali ya miongo kadhaa iliyopita katika ukuta wa eneo lote Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) yanaweza kuzua vita vya kidini katika eneo hilo.

Onyo hilo limetolewa na Idara ya Wakfu ya Kiislamu, inayosimamia Msikiti wa Al-Aqsa na maeneo matakatifu ya Waislamu mjini Quds.

Indhari hiyo  limekuja baada ya miito ya hivi majuzi ya vikundi vya Kiyahudi vyenye itikadi kali kuingia katika moja ya maeneo ya Msikiti wa Al Aqsa na kufanya ibada za Kiyahudi hapo kuanzia Jumapili.

Makundi ya Kiyahudi na Kizayuni yenye itikadi kali yanataka kuugeuza eneo la Msikiti wa Al Aqsa amalo liko karibun na lango la Bab al-Rahmah (Lango la Dhahabu) kuwa hekalu la Kiyahudi, ikiwa ni hatua ya kuuyahudisha Msikiti wa Al-Aqsa katika hali ambayo msikiti huo wote ni wa Waislamu na haiwezekani kuugawa.

Idara ya Wakfu ya Kiislamu, inayosimamia Msikiti wa Al-Aqsa imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel usithubutu kuruhusu jumuiya za Kiyahudi zenye itikadi kali kuingia katika eneo hilo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu kwani kufnaya hivyo niswa na kuzusha na  kuchochea mzozo.

Idara hiyo imesema miito hiyo ya mashirika yenye itikadi kali "italiingiza eneo hilo katika vita vya kidini vyenye matokeo ya kutisha," ambayo Israel itabeba dhima yake, na kusisitiza kwamba "watu wa Quds, Palestina na Waislamu wote hawatasita kuulinda Msikiti wao.”

Utawala wa Kizayuni na Mayahudi wenye kufurutu mipaka huamini kuwa Msikiti wa Al Aqsa ni milki yao na hivyo kipaumbele cha kuingia katika msikiti huo mtakatifu kinapaswa kupewa Mayahudi. Ni kutokana na itikadi hiyo potovu ndio kunatekelezwa njama ya Kuuyahudisha Msikiti wa Al Aqsa na kupotosha historia sambamba na kupuuza haki za Wapalestina.

Ili kuweka mambo wazi , mwaka 2016, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) lilipasisha azimio na kusema Mayahudi hawahusiki kivyovyote vile na maeneo matakatifu ya Quds ukiwemo Msikiti wa al Aqsa. Azimio hilo la UNIESCO lilisema wazi kuwa, maeneo hayo matakatifu ni ya Waislamu. Aidha Kamati ya Nnne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 202 ilipasisha azimio ambalo liliungwa mkono na nchi 139 na kutangaza kuwa, Msikiti wa Al Aqsa una utambulisho kamili wa Kiislamu na hauna uhusiano wowote na Mayahudi.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukipuuza nyaraka za kihistoria na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukweli kuwa Msikiti wa Al Aqsa ni milki ya Waislamu. Upuuzaji huo ndio chanzo cha Israel kuendeleza sera zake za kutumia mabavu na ukatili dhidi ya Wapalestina ili kuwazuia kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa ambao pia unajulikana kama  Al-Haram Al-Sharif.

3479539

Kishikizo: al aqsa ، quds ، palestina ، mayahudi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha