IQNA

Sunni na Shia

Urithi wa Imam Sadiq (AS) katika ulimwengu wa Kiislamu

16:12 - May 26, 2022
Habari ID: 3475297
TEHRAN (IQNA) - Imam Sadiq (AS) ni mmoja wa shakhsia mashuhuri wa elimu na sayanzi za Kiislamu katika nyanja mbalimbali kama vile fiqhi, tafsiri, maadili, jiografia, uchumi, unajimu, tiba na hisabati, ambapo wanafunzi wake waliibua uwezo mkubwa katika maendeleo ya elimu na sayansi katika kote katika ulimwengu wa Kiislamu.

Ja'far bin Muhammad al-Sadiq, mmoja wa wajukuu wa Mtume Mtukufu amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na Ali zake, ambaye ni maarufu kama Imam Sadiq (AS), alizaliwa mnamo tarehe 17 Rabiul Awwal mwaka 83 Hijria Qamariya (702 Miladia).

Kipindi cha maisha yake kilikuwa zama za kuchanua elimu na maarifa, tafsiri ya Qur'ani na kusambaa elimu mbalimbali. Katika kipindi cha miaka 65 ya maisha yake, alikuwa na sifa kubwa ya umahiri wa kielimu na kisayansi katika nchi za Kiislamu, kiasi kwamba, watu kutoka nchi mbalimbali walikuja kwake ili kupata elimu. Aliwafunza na kuwalea wanafunzi wengi, na mmoja wao ni Jabir ibn Hayyan (karne ya sita Miladia) ambaye anajulikana kama baba wa kemia. 

Hatimaye, tarehe 25 Shawwal mwaka 148 Hijria Qamaria, Imam Sadiq (AS), ambaye ni Imamu wa sita wa Mashia, aliuawa shahidi.

Viongozi wa madhehebu za  Kisunni ni miongoni mwa wanafunzi wake maarufu, kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, na wameeleza yafuatayo kuhusu shakhsia ya kimaadili na kileimu ya Imam Sadiq (AS), ambayo baadhi yake tutayasoma hapa chini:

Imam Malik Ibn Anas

Muhammad bin Ziad anasema: Nilimsikia Malik bin Anas akisema: Sijapata kumuona isipokuwa katika hali tatu nzuri; "Ima aliswali, au alikuwa amefunga, au alikuwa akisoma Qur'ani, na daima alikuwa akizungumzia wema na utakasifu."

Imam Abu Hanifa

Imam Abu Hanifa ni mmoja wa wanafunzi wa Imam Ja'far Sadiq (AS) ambaye alisema hivi kumhusu mwalimu wake: "Sijapata kumuona mwanasheria (mwanafaqihi) aliyebobea na mjuzi zaidi kuliko Ja'far bin Muhammad." Mahali pengine anasema: "Kama si Ja'far Ibn Muhammad (AS), watu wasingelijua kuhusu Hija na utaratibu wa ibada hii."

Khair al-Din al-Zarqali

Khair al-Din al-Zarqali ni mwandishi mwingine wa Kisunni ambaye ameacha maandishi muhimu katika kumbukumbu yake. Ameandika katika kitabu chake "Al-Alam" kuhusu Imam Ja'far al-Sadiq (AS): "Imam Ja'far al-Sadiq (as) ana hadhi ya juu katika sayansi na elimu na watu wengi wamepata elimu kutoka kwake, wakiwemo viongozi wawili wa Kisunni ambao ni Imam Abu Hanifa na Imam Malik. Lakabu yake Imam Sadiq (AS) ni 'Mkweli'  kwa sababu hakuna mtu aliyewahi kusikia uwongo kutoka kwake.

3975764

captcha