Anashtakiwa kwa uchochezi dhidi ya kaumu, na kumfanya kuwa mtu wa kwanza kwenda kupandishwa kizimbani Usiwdi kuhusiana na tukio hilo.
Kulingana na ripoti ya The Guardian, Paludan, kiongozi wa chama cha kisiasa cha Stram Kurs (Msimamo MkALI), alikataa kuhudhuria mahakama ya wilaya ya Malmö wakati kesi ilipoanza Jumatatu, akisema maisha yake yangekuwa hatarini ikiwa angeenda katika mji wa kusini mwa Uswidi.
Badala yake, alionekana kupitia video kutoka eneo lisilojulikana nchini Uswidi, iliongeza ripoti hiyo.
Paludan, 42, anakabiliwa na makosa mawili ya uchochezi dhidi ya kaumu na shtaka moja la matusi yanayohusiana na matukio yaliyofanyika nchini Uswidi mnamo 2022, iliripoti The Guardian.
Mnamo Aprili 2022, aliendesha mkutano wa hadhara ambao ulichochea ghasia katika miji kadhaa ya Uswidi, ikiwemo Malmö, Landskrona, Linköping, na Örebro, wakati wa wikendi ya Pasaka. Mwendesha mashtaka anasema kauli zilizotolewa na Paludan katika mkutano huu zilijumuisha uchochezi dhidi ya kabila.
Katika tukio tofauti mnamo Septemba 2022, alidaiwa kufanya mashambulizi ya maneno yaliyochochewa na ubaguzi wa rangi kwa "Waarabu na Waafrika," na hivyo kukabiliwa na mashtaka ya matusi, ambayo chini ya sheria za Uswidi yanaweza kusababisha faini au hadi miezi sita jela.
Paludan, hata hivyo, amekanusha mashtaka yote dhidi yake.
Vilhelm Persson, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Lund, aliiambia The Guardian kwamba kesi ya Paludan ina "umuhimu wa kimsingi" kama kesi ya kwanza inayohusiana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi.
3490289