IQNA

Udhalimu wa Israel

Askari wa utawala wa Kizayuni wabomoa nyumba za Wapalestina, Al Quds

21:27 - June 22, 2022
Habari ID: 3475412
TEHRAN (IQNA) - Nyumba za Wapalestina zilibomolewa na wanajeshi wa utawala dhalimu Israel huko Al-Quds (Jerusalem) na mji wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah siku ya Jumatano.

Matinga ya utawala dhalimu wa Israel yalibomoa nyumba na ghala la Wapalestina katika kitongoji cha Al-Quds  cha Al-Isawiya

Katika kijiji cha Nilin, magharibi mwa Ramallah, nyumba iliyokuwa bado inajengwa ilibomolewa baada ya wanajeshi katili wa Israel kuvamia kijiji hicho, shirika la habari la Mamlaka ya Ndani ya Palestina Wafa liliripoti.

Nyumba hizi zilibomolewa kwa kisingizio cha wamiliki kutokuwa na kibali.

Vikosi vya utawala vamizi na wa kikoloni wa Israel pia viliwakabidhi Wapalestina wanane kutoka kijiji cha Jalboun, mashariki mwa Jenin notisi ya kusimamisha ujenzi wa nyumba na kumpa Mpalestina mwingine notisi ya kubomoa nyumba yake mwenyewe ndani ya muda wa saa 96.

Iwapo Wapalestina watakataa kufuata amri za utawala dhalimu wa Israel za kubomoa nyumba yao wenyewe, mamlaka ya Israel mara nyingi hubomoa nyumba na kuwapiga wamiliki kwa faini kubwa kama adhabu.

Huku Israel ikikataa kutambua aina za kitamaduni za umiliki wa nyumba na ardhi za Wapalestina, Wapalestina wameamua kuomba vibali vya ujenzi kutoka kwa mamlaka za Israel ili kufanya umiliki wa ardhi yao rasmi.

Kukataa kwa mara kwa mara kwa Israel kutoa vibali kunamaanisha kuwa inakataa kutambua haki za Wapalestina kwa makazi yao wenyewe katika eneo linalokaliwa kwa mabavu.

Gharama ya kibali cha nyumba moja inakadiriwa kuwa katika eneo la $30,000.

Bei za ulaghai za vibali vya ujenzi, ambazo Wapalestina wengie hawazimudu , huzua mwanya wa kisheria kwa Israel kunyakua ardhi zaidi na kuwazuia Wapalestina kuendeleza miundombinu.

Ukingo wa Magharibi, ambao umekaliwa kwa mabavu na wanajeshi wa Israel tangu vita vya siku sita vya mwaka 1967, ni makazi ya walowezi wapatao 600,000 wa Kizayuni

3479422

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha