IQNA

Jinai za Israel

Jihadi Islami: Wapalestina hawatawasahau Mashahidi

18:39 - July 24, 2022
Habari ID: 3475533
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Jihad Islami (Jihadi ya Kiislamu) ya Palestina imelaani vikali jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umewaua vijana wawili Wapalestina na kusema ukatili kama huo hauwezi kuvuruga azma ya Wapalestina kupigiania ukombozi wao.

"Cheche za mapambano na muqawama zitaendelea kuutukisa usalama wa utawala wa Kizayuni," imesema taarifa ya Jumapili ya Jihad Islami.

Taarifa hiyo imesema Wapalestina katu hawatasahau damu ya mashahidi wao na wataendeleza mapambano hadi ukombozi wa ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mauaji ya vijana hao pia yamelaaniwa vikali na Harakati ya Mapambano ya Palestina, (Hamas) na Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina wawili na kujeruhi wengine 19 katika miji ya Nablus na Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ma'an la Palestina, Wapalestina hao wameuawa na kujeruhiwa mapema leo baada ya wanajeshi makatili wa Israel kuvamia miji hiyo ya Ukingo wa Magharibi.

Ma'an imeripoti kuwa, Aboud Sobh, aliyekuwa na umri wa miaka 29, na Muhammad Al-Azizi aliyekuwa na miaka 22 wameaga dunia wakitibiwa katika Hospitali ya Rafidia mjini Nablus, baada ya kumiminiwa risasi na Wazayuni.

Raia 19 wa Palestina waliojeruhiwa kwenye muendelezo huo wa chokochoko za askari vamizi wa Israel wanaendelea kutibwa hospitalini.

Wanajeshi wa Kizayuni mapema leo wamevamia mji mkongwe wa Nablus kutoka maeneo kadhaa na kisha kulizingira eneo la Al Yasmina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Hata hivyo wavamizi hao wa Kizayuni wamekabiliwa vikali na wanamuqawama wa Palestina kwa saa tatu na hatimaye wakalazimika kukimbia.

Katika wiki za hivi karibuni, wanajeshi makatili wa Israel wameshadidisha hujuma na mashambulizi yao dhidi ya miji ya Wpalestina, wakitokea Ukingo wa Magharibi.

3479824

captcha