IQNA

Waislamu India

Maandamano yazuka baada ya msikiti kubomolewa Hyderabad, India

15:33 - August 03, 2022
Habari ID: 3475572
TEHRAN (IQNA) - Maandamano yamezuka baada ya msikiti katika viunga vya Hyderabad nchini India kubomolewa na manispaa ya mji huo.

Masjid-e-Khwaja Mahmood katika Green Avenue Colony ya Shamshabad ulibomolewa na wafanyikazi wa manispaa wakiwa wanalindwa na polisi.

Tukio hilo lilisababisha maandamano makubwa ya Waislamu na viongozi wa vyama mbalimbali katika eneo hilo.

Viongozi wa jumuiya za Waislamu India za  All India Majlis-e-Ittehadul Muslimeen (AIMIM) na Majlis Bachao Tehreek (MBT) waliwasilisha maandamano yao.

Kiongozi wa MBT Amjadullah Khan alisema msikiti huo ulijengwa miaka mitatu iliyopita na kila siku sala tano husaliwa hapo pamoja na  Sala ya Ijumaa kila wiki.

Alisema kuwa ardhi ya  eneo Green Avenue Colony yenye ekari 15 za ardhi ilipangwa na kuuzwa baada ya ruhusa kutoka kwa Shamshad Grampanchayat. Viwanja viwili vya yadi za mraba 250 viliwekwa alama kama eneo la msikiti.

Mtu ambaye nyumba yake iko kando ya msikiti huo, pamoja na baadhi ya wakazi wengine, walilalamika kwa mamlaka ya Manispaa ya Shamshad dhidi ya ujenzi wa msikiti huo.

Kiongozi wa MBT alisema ingawa kesi ilikuwa mahakamani, mamlaka ya manispaa iliamua kubomoa, na kuumiza hisia za kidini.

Viongozi wa eneo la AIMIM pia walifanya kikao katika ofisi ya manispaa. Walitaka wachukuliwe hatua maafisa waliohusika kuubomoa na kuujenga upya msikiti huo mara moja.

Polisi baadaye waliwakamata waandamanaji waliokuwa wakiongozwa na AIMIM incharge wa eneo bunge la Rajendra Nagar, Mirza Rahmat Baig.

Viongozi wa Kiislamu wamelaani ubomoaji huo na kuitaka serikali ya Telangana Rashtra Samithi (TRS) kuchukua hatua za haraka dhidi ya waliohusika.

Kiongozi wa MBT Khan alisema kuwa serikali ya TRS inayoongozwa na KCR imekuwa ikifuata nyayo za serikali ya Yogi ya BJP. Alidai tangu chama cha TRS kiingie madarakani mwaka 2014, misikiti sita ilibomolewa huko Telangana.

Alihoji ukimya wa mashirika hayo ya Waislamu na wanasiasa wanaodai KCR kama kiongozi wa kidini. Alisema ubomoaji huo ulifanywa na Idara ya Manispaa inayoongozwa na mtoto wa KCR K.T. Rama Rao.

3479954

Kishikizo: Hyderabad india waislamu
captcha