IQNA

Hali ya Waislamu India

HRW :Kumeongezeka ukandamizaji wa Waislamu nchini India

19:24 - October 07, 2022
Habari ID: 3475891
TEHRAN (IQNA) – Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa mamlaka nchini India zinazidi kuwakandamiza na kuwaadhibi Waislamu nchini humo.

Katika majimbo kadhaa yanayotawaliwa na Chama tawala chenye misimamo mikali ya Kihindu cha Bharatiya Janata (BJP), mamlaka imebomoa nyumba na mali za Waislamu bila idhini ya kisheria, na hivi majuzi zaidi, waliwachapa viboko Waislamu hadharani wanaotuhumiwa kuvuruga tamasha la Kihindu.

"Watawala katika majimbo kadhaa ya India wanawakandamiza  Waislamu i," alisema Meenakshi Ganguly, mkurugenzi wa Asia Kusini katika Human Rights Watch. "Viongozi wanaopuuza waziwazi utawala wa sheria wanatuma ujumbe kwa umma kwamba Waislamu wanaweza kubaguliwa na kushambuliwa."

Mwezi Juni, wataalamu  wa Umoja wa Mataifa waliiandikia serikali ya India wakielezea wasiwasi wao kwamba "kufukuzwa kumefanywa kama aina ya adhabu ya pamoja na ya kiholela dhidi ya Waislamu walio wachache.”

Ubomoaji wa nyumba na maeneo ya  Waislamu umeongeza hatari ya wanawake, watoto, wazee, na watu wenye ulemavu wanaoishi huko, Human Rights Watch ilisema.

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, ambao India imeuidhinisha, unakataza ubaguzi kwa misingi yoyote na hulazimisha mataifa kuhakikisha kuwa kila mtu ni sawa mbele ya sheria na kuhakikisha ulinzi sawa wa sheria. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni unahakikisha haki ya kiwango cha kutosha cha maisha, ikiwa ni pamoja na makazi ya kutosha.

Katika Maoni yake ya, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni, chombo huru cha wataalam ambacho kinafuatilia utiifu wa mkataba huo, ilibainisha kuwa ubomoaji wa nyumba ni hatua ya adhabu iliyo kinyume cha mkataba huo.

3480747

"

Habari zinazohusiana
Kishikizo: waislamu india bjp
captcha