IQNA

Waislamu India

Kundi la Kiislamu la PFI lapigwa marufuku India

18:57 - September 29, 2022
Habari ID: 3475852
TEHRAN (IQNA)- India imeipiga marufuku harakati mashuhuri ya Kiislamu nchini humo ya PFI, ikiwa ni muendelezo wa serikali ya New Delhi ya kufuata sera ya kukanyaga na kupuuza haki za Waislamu walio wachache katika nchi hiyo.

Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya India imetangaza kuwa, imeipiga marufuku harakati ya Popular Front of India (PFI) pamoja na makundi yake tanzu kwa muda miaka mitano. PFI ndilo kundi kubwa zaidi la kisiasa linalowakilisha na kutetea maslahi ya Waislamu nchini India.

Taarifa hiyo imeitaja PFI kama kundi haramu, pamoja na harakati zake tanzu zikiwemo za Rehab India Foundation, Campus Front of India, All India Imams Council, National Confederation of Human Rights Organisation, National Women’s Front, Junior Front na Empower India Foundation miongoni mwa nyingine.

Katika miaka ya hivi karibuni, sera za ubaguzi za chama tawala nchini India dhidi ya Waislamu, zimewahamasisha Wahindu wenye misimamo mikali kuzidisha vitendo vya chuki na hujuma dhidi ya wafuasi wa dini hiyo ikiwemo kuharibu maeneo matakatifu na kuzidisha mateso na manyanyaso dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali. 

Historia ya chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP) nchini India katika kuvunjia heshima matukufu ya kidini ya Waislamu, ikiwa ni pamoja na kushambuliwa na kuharibu misikiti yao, ni moja ya nukta za giza za utendaji wa chama hicho katika miongo miwili iliyopita.

Mara kwa mara, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imekuwa ikitoa taarifa za kulaani vitendo vya kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu nchini India.

3480648

Kishikizo: india ، waislamu ، BJP ، PFI
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha