IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Wanazuoni wa Kiislamu duniani wataka marufuku kutukanwa matukufu ya kidini

12:41 - June 20, 2022
Habari ID: 3475402
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa mwito wa kupasishwa sheria ya kujinaisha na kupiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya dini mbalimbali duniani.

Taasisi hiyo ya kidini yenye makao makuu yake Doha, mji mkuu wa Qatar imesema itatuma ujumbe wa wasomi wa Kiislamu kuzitembelea nchi za Waislamu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na midahalo kuhusu kushtadi kesi za kuvunjiwa heshima dini tukufu ya Kiislamu.

Taarifa ya IUMS imesema, taasisi hiyo ya kimataifa ya wanazuoni wa Kiislamu itaiomba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Umoja wa Mataifa zishinikize kupasishwa sheria ya kukabiliana na hatua yoyote inayovunjia heshima thamani na matukufu ya dini za Mbinguni.

Haya yanajiri wakati huu ambapo mataifa ya Kiislamu yanaendelea kulaani kitendo cha wanasiasa wa chama tawala nchini India cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na matukufu ya Kiislamu.

Kufuatia chokochoko hizo, Qatar, Kuwait na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ziliwaita mabalozi wa India katika nchi hizo, kulalamikia hatua hiyo ya kumvunjia heshima Bwana Mtume SAW.

Hivi karibuni pia, Mamosta Abdul Salam Karimi, Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya jamii za wachache nchini Iran sambamba na kulaani jinai ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Sweden alisema kuwa, leo hii jamii ya mwanadamu inahitajia mno amani, usalama, kuishi pamoja na utulivu, mantiki na kuheshimiana, na kwamba vitendo kama vilivyotokea huko Sweden ni uchochezi wa wazi wa vurugu na machafuko.

Hivi karibuni, Sheikh Dkt. Ali Mohyiddeen Al-Qaradaghi katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu aliashiria kuhusu jinai wanagambo wa Kihindu wenye misimamo mikali ya wanawakandamiza Waislamu nchini India "Natoa wito wa kuundwa harakati ya kimataifa ya kisheria kwa ajili ya kulinda haki za Waislamu wanaoishi kama jamii za waliowachache maeneo mbali mbali duniani."

3479370

captcha