IQNA

Maombolezo ya Imam Hussein AS

Mijumuiko ya 'Vichanga Vinyonyavyo vya Imam Hussein (AS)' imefanyika leo

18:59 - August 05, 2022
Habari ID: 3475581
TEHRAN (IQNA0- Mijumuiko maalumu wa 'Vichanga Vinyonyavyo vya Imam Hussein (AS)' Imefanyika leo sambamba na Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram katika maeneo 7,500 nchini Iran na katika nchi zingine 45 duniani.

Kila mwaka na katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram, kwa mnasaba wa kukumbuka alivyouawa shahidi kikatili Ali Asghar, mtoto mchanga wa miezi sita wa Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani, hufanyika kongamano na mjumuiko maalumu unaoshirikisha akina mama na watoto wao wachanga wanaonyonya.

Mijumuiko hiyo ijulikanayo kama 'Vichanga Vinyonyavyo vya Imam Hussein (AS)' , imefanyika kote nchini Iran na katika nchi zingine duniani ikiwemo India, Pakistan, Bahrain, Iraq, Saudi Arabia, Uturuki, Afghanistan, Nigeria  n.k, ambapo akina mama wamewawekea nadhiri watoto wao kwa ajili ya mapambano ya Imam wa Zama, Imam Mahdi (AS), ambaye ni Imamu wa 12 na wa mwisho wa Waislamu wa Kishia.

Hapa mjini Tehran, shughuli hiyo imefanyika katika Uwanja Mkuu wa Sala wa Imam Khomeini (MA), ambapo akina mama waliokuwa wamebeba watoto wao wachanga waliomboleza masaibu na mateso yaliyompata Imam Hussein (AS).

Imam Hussein (AS) ambaye kwa kujitolea kwake mhanga kusio na kifani aliuawa shahidi Siku ya Ashura, yaani tarehe 10 Muharram katika ardhi ya Karbala, amewaachia walimwengu wote somo kubwa la maana halisi ya kukomboka na kuwa na izza na heshima.

Katika siku hiyo ya Ashura katika jangwa la Karbala Imam Hussein (AS) alisisitiza kuwa: "kusudio langu ni kuufedhehesha utawala ulio dhidi ya Uislamu, kuamrisha mema na kukataza maovu na kusimama dhidi ya dhulma na uonevu".

Mafunzo yaliyomo kwenye harakati ya Imam Hussein (AS) yamevuka mipaka ya historia na jiografia na kujumisha wanadamu wote ulimwenguni.

Mausoleum of Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) in TehranMausoleum of Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) in TehranMausoleum of Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) in TehranMausoleum of Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) in TehranMausoleum of Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) in TehranMausoleum of Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) in Tehran
 
Mosalla of SemnanMosalla of SemnanMosalla of SemnanMosalla of SemnanMosalla of SemnanMosalla of Semnan
 
AhvazAhvazAhvazAhvazAhvazAhvaz
 
EsfahanEsfahanEsfahanEsfahanEsfahanEsfahan
 
Imam Reza (AS) holy shrine in MashhadImam Reza (AS) holy shrine in MashhadImam Reza (AS) holy shrine in Mashhad
 
Tehran's MahdiehTehran's MahdiehTehran's MahdiehTehran's MahdiehTehran's MahdiehTehran's Mahdieh
 
Shah Cheragh Mausoleum in ShirazShah Cheragh Mausoleum in ShirazShah Cheragh Mausoleum in ShirazShah Cheragh Mausoleum in ShirazShah Cheragh Mausoleum in ShirazShah Cheragh Mausoleum in Shiraz
 
ZanjanZanjanZanjanZanjanZanjanZanjan
 
 
 
 

3479985

Kishikizo: ASGHAR ، imam hussein as ، vichanga
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha