IQNA

Mazishi ya Kimbari: Mashahidi 112 wazikwa katika mkusanyiko mkubwa Gaza

16:21 - August 05, 2026
Habari ID: 3482590
IQNA – Katika tukio la kusikitisha na la kihistoria, miili ya mashahidi 112 imezikwa katika mazishi makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kushuhudiwa katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina, Shehab, wananchi wa Gaza siku ya Jumanne waliwaaga mashahidi kutoka familia za Abu Sharia na Al-Hassayanah. Miili hii ilifukuliwa kutoka katika vifusi vya jengo la makazi lililoharibiwa kwa mabomu ya Utawala wa Kizayuni wa Israel mnamo Novemba 22, 2023. Mauaji haya ya kinyama yaligharimu maisha ya Wapalestina 308, huku miili mingine ikisalia chini ya kifusi na mingine ikiwa imepotea kabisa kutokana na ukubwa wa mashambulizi ya mabomu.

Hili linatajwa kuwa miongoni mwa mauaji ya kimbari yenye maumivu makali zaidi kutokana na operesheni za kijeshi za utawala huo dhalimu dhidi ya Gaza. Familia nyingi bado zinangoja kwa matumaini na hofu habari za wapendwa wao walipotea, huku juhudi za uokoaji zikiendelea katika maeneo mbalimbali yaliyoharibiwa.

Akihutubia ulimwengu wakati wa mazishi hayo, Mahmoud Basal, msemaji wa Idara ya Uokoaji ya Gaza, aliuliza kwa masikitiko: “Enyi watu wa dunia, kwa nini watoto hawa wanauawa Gaza? Enyi watu huru wa dunia, tuambieni!”

Kilio hiki ni ushahidi mwingine wa dhulma inayopaswa kusitishwa, na msimamo wetu kama wapigania haki unabaki imara katika kuunga mkono muqawama na mashahidi wa Palestina.

3498539

Habari zinazohusiana
captcha