IQNA

Ashura

Mapambano ya Ashura yanahamasisha ukombozi

23:21 - August 06, 2022
Habari ID: 3475587
TEHRAN (IQNA) – Mwamko Ashura ni kielelezo cha kipekee cha mapambano dhidi ya mifumo mbovu ya kisiasa na njia mbovu za utawala.

Katika zama za kisasa, wapigania uhuru wa Kiislamu na hata watu kama hao na viongozi wa harakati za uhuru kama Mahatma Gandhi wametiwa moyo na Ashura.

Miaka 1383 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, tarehe 10 mwezi wa Muharram moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq.

Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu. Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya. Pili ni upeo wa ukatili, udhalimu na unyama ulioonyeshwa na jeshi batili la Yazid bin Muawiya. Baada ya kupambana kishujaa, hatimaye mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW aliuawa shahidi katika siku kama ya leo.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) limemuuliza mwanachuoni wa wa chuo cha Kiislamu  Hujjatul-Islam Seyed Ali Mirmousavi kuhusu mafunzo ya tukio la Ashura.  

IQNA: Wakati dunia inakabiliwa na changamoto za wanaounga mkono mfumo wa kisekula na jamii ya kisasa na ubinadamu unakabiliwa na migogoro mbalimbali kama ile inayohusiana na utambulisho, maadili na hali ya kiroho, ni mafunzo na ujumbe gani yaliyomo katika mwamko wa Ashura kwa ajili ya kuokoa ubinadamu na jamii kutokana na hali hii?

Hujjatul-Islam Mirmousavi: Ashura ni kielelezo cha kipekee cha mwamko dhidi ya mifumo mbovu ya kisiasa na njia mbaya za utawala. Katika zama za kisasa, wapigania uhuru wa Kiislamu na hata watu kama vile Mahatma Gandhi ambaye aliongoza harakati za ukombozi, wametiwa moyo na tukio la Ashura. Maadili, kuthamini uhuru na kutafuta uhuru vinadhihirika katika mwamko wa Ashura. Mafunzo ambayo Ashura inayo kwa ubinadamu wa kisasa ni pamoja na yale yanayohusiana na maadili ya mwamko na mapambano, kuthamini uhuru na ukombozi. Mwamko wa Imam Hussein (AS) haukuwa kwa vyovyote vile hatua ya vurugu  au ghasi. Imam Hussein (AS) alifikiria kila hatua ya kuzuia vita na migogoro na akakimbilia tu upanga pale alipokabiliwa na chaguo kati ya fedheha na kufa shahidi.

 

IQNA: Ni vipi tukio la Ashura linaweza kuchambuliwa kwa kuzingatia fikra ya jamii timilifu au utopia?

Hujjatul-Islam Mirmousavi: Suala la jamii timilifu na itikadi ni muhimu. Jamii timilifu inamaanisha kuwasilisha taswira ya hali bora na kutafuta jamii timilifu kwa lengo la kukosoa hali ya sasa na kuibadilisha kuwa bora. Jamii timilifu imekuwa miongoni mwa masuala yanayopewa umuhimu na vikosi vya wanamapinduzi na hivyo fikra ya kutaka kuunda jamii timilfu ndio huibua mapinduzi daima. Kwa upande mwingine kuna itikadi. Itikadi ni tafsiri ambayo muundo wake unawasilisha ukweli na inaendana na kutetea matumizi ya nguvu na madaraka. Ama kuhusu tukio la Ashura, kuna mtazamo wa jamii timilifu na mtazamo wa kiitikadi. Katika hatua ya kwanza, mwamko wa Imam Hussein (AS) ni mfano wa kuigwa kwa ajili ya kupinga hali iliyopo na mapambano dhidi ya utawala wa kiimla ulio madarakani. Utawala huo wa kiimla ulikuwa ni wa Yazid na, kwa hivyo, kukabiliana na utawala huo kunachukuliwa kuwa jukumu na mfano huo unatumika katika zama zetu hizi.

Katika tafsiri ya wajibu, kwa kuzingatia hali tofauti za kihistoria, umuhimu unaambatanishwa na vipengele vya msukumo na mfano wa harakati. Hivyo mwamako wa Imam Hussein (AS) ulikuwa wajibu begani mwake katika wakati fulani wa kihistoria. Imam (AS) aliwakumbusha wale ambao walitaka kumtahadharisha kuhusu kitakachomtokea wakati wa kutekeleza wajibu wake. Katika mtazamo wa Imam (AS), umuhimu na thamani ya jukumu hili lilikuwa kwamba asingeweza kuliacha pamoja na kuwafahamu hatima ambayo ingemkumba. Nukta ya kipekee ya mwamako wa Imam Hussein (AS) katika historia ya ubinadamu ni kwamba alijitoa muhanga katika njia ya kutekeleza wajibu huu. Ingawa Imam (AS) alijaribu kufanya mwamko wake uwe na gharama ndogo kadiri iwezekanavyo, alipokabiliwa na chaguo kati ya maisha ya fedheha na kufa shahidi, alichagua la pili. Katika zama za kisasa, pia, wengi wa wale ambao wamekubali gharama ili kutimiza wajibu wao wanatazama Ashura kwa mtazamo huu.

Kishikizo: ashura ، imam hussein as ، karbala
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha