IQNA

Jinai za Israel

Utawala katili wa Israel umewaua watoto 6 Wapalestina katika hujuma Gaza

15:18 - August 07, 2022
Habari ID: 3475589
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya Wapalestina waliouliwa shahidi katika jinai zinazoendelea za utawala wa Kizayuni huko Gaza imeongezeka na kufikia watu 24 wakiwemo watoto wadogo sita.

Utawala katili wa Israel unaoua watoto wadogo bila kiwewe, ulianzisha mashambulizi makubwa juzi Ijumaa dhidi ya maeneo ya makazi ya watu huko Gaza na hadi leo Jumapili, mashambulio hayo yanaendelea.

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imesema kuwa, idadi ya Wapalestina waliouwa shahidi walikuwa ni 24 wakiwemo watoto wadogo 6 na wengine 215 walikuwa wamejeruhiwa hadi wakati inatangaza habari hiyo.

Ijumaa alasiri, jeshil la utawala wa kigaidi wa Israel lilitekeleza jinai kubwa dhidi ya Wapalestina kupitia mashambulizi yaliyopewa jina la "Operesheni ya Alfajiri", katika maeneo yanayodhibitiwa na harakati ya Palestina ya Jihad Islami katika Ukanda wa Gaza.

Katika jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni, Wapalestina 12 akiwemo mtoto wa miaka 5, pamoja na Taysir al-Jabari, kamanda wa eneo la kaskazini katika Brigedi ya Quds, waliuawa shahidi. Katika mashambulizi hayo ya utawala wa Kizayuni, maeneo ya kundi la Jihad Islami la Palestina na wanachama wake walilengwa. Al-Ja'bari, ambaye alichaguliwa kama mrithi wa Shahidi Baha Abul Ata mnamo mwaka 2019, alinusurika majaribio mawili ya mauaji mnamo 2012 na 2014. Al-Jabari alikuwa kamanda wa eneo la kaskazini la Brigedi ya al-Quds katika operesheni ya "Upanga wa al-Quds" mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa wasimamizi wa uundaji wa makombora ya harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu, ukiwemo mfumo wa makombora wa Jihad al-Islami uliozinduliwa mwezi Mei 2021.

Kwa kumuua al-Jabari, utawala huo wa Kizayuni umetaka kulipiza kisasi cha oparesheni ya mwaka uliopita ya Upanga wa al-Quds na wakati huo huo kumfuta mmoja wa makamanda muhimu wa Jihad Islami. Mbali na al-Jabari, utawala wa Kizayuni umewatia mbaroni makumi ya wanachama wa harakati hiyo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Gazeti la Kizayuni la Maariv limedai kuwa, Wapalestina hao walihusika katika operesheni tofauti dhidi ya utawala wa Israel.

Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika maeneo ya ya Jihad Islami ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza yametekelezwa kwa mara nyingine tena huku mwenendo wa uchaguzi wa utawala huo ukikabiliwa na mkwamo wa kisiasa. Vita vya siku 12 vya mwaka jana pia vilitokea baada ya waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda baraza la mawaziri. Sasa baraza la mawaziri la muungano wa Lapid na Bennett limeporomoka na uchaguzi mwingine wa bunge umepangwa kufanyika Novemba ijayo.

3480003

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha