IQNA

Jinai za Israel

Zaidi ya Wapalestina zaidi ya 110 wauawa na Israel Mwaka huu

21:02 - September 02, 2022
Habari ID: 3475723
TEHRAN (IQNA) – Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limeua Wapalestina zaidi ya 110 na wengine wengi kujeruhiwa hadi sasa mwaka huu.

Katika  taarifa, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Palestina, "Hadi sasa mwaka 2022, mashambulizi ya Jeshi la Utawala wa Israel yaliwaua Wapalestina 111, watoto 24 na wanawake 8.

Aidha taarifa hiyo imebaini kuwa, takriban Wapalestina 1,277 walijeruhiwa, wakiwemo watoto 195, wanawake 39 na waandishi wa habari 22, huku Wapalestina watatu, akiwemo mwanamke mmoja, wakifariki dunia katika magereza ya Israel katika kipindi hicho, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeongeza kuwa mwaka huu pekee, jeshi la Israel limeharibu nyumba za  familia 108 zenye watu 648 wakiwemo wanawake 123 na watoto 300 kutokana.

Vikosi vya utawala dhalimu wa Israel pia vimeharibu majengo 81 ya kiraia, vimeharibu maeneo makubwa ya ardhi, vimewasilisha notisi nyingi za kubomoa, kusimamisha ujenzi wa mali za Wapalestina na kutoa notisi za kufukuzwa.

Walowezi wa Kiyahudi wenye itikadi kali walifanya mashambulizi yasiyopungua 176 dhidi ya Wapalestina, na kuua raia wawili.

Halikadhalika ripoti hiyo imebaini kuwa, vikosi vya Israel vilifanya mashambulizi 185 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ikiwa ni pamoja na al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, ambapo walivamia na kupekua makazi na vituo vya Wapalestina.

Wakati wa uvamizi huo, Wapalestina 73 wakiwemo watoto wanane walikamatwa.

"Utawala vamizi wa Israel unaendelea na mzingiro wake wa kinyama na usio halali uliowekwa kwenye Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miaka 15 na unaendelea kuweka vikwazo kwa uhuru wa kutembea katika Ukingo wa Magharibi," imesema ripoti hiyo.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Palestina iliitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jina, ICC,  kuchukua hatua kwa umakini kuhusiana na hali ya Palestina sawa na hatua yake ya haraka nchini Ukraine.

3480316

Kishikizo: israel palestina jinai
captcha