IQNA

Watoto na Wanawake ni 70% ya waliouawa na Israel katika vita vya Gaza

12:58 - December 18, 2023
Habari ID: 3478053
IQNA Ripoti ya kutisha iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina, imefichuliwa kuwa wakati wa hujuma za hivi karibuni za kijeshi za utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, asilimia 70 ya watu 18,800 waliouawa walikuwa wanawake na watoto.

Takwimu za kutisha zinahusu kipindi cha kikatili cha siku 70 kutoka Oktoba 7 hadi Desemba 15, zikitoa picha mbaya ya mauaji ya kimbari katika eneo hilo la Palestina lililozingirwa.

Wizara ya Afya ya Palestina ilifichua kuwa miongoni mwa waathirika walikuwa zaidi ya wafanyakazi 300 wa sekta ya afya, waandishi wa habari 86, wafanyakazi 135 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Wapalestina, UNRWA, na takriban wafanyakazi 35 wa ulinzi wa raia.

Zaidi ya Wapalestina 51,100 wamejeruhiwa, na idadi kubwa ya watu bado hawajulikani waliko.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Gaza Ashraf al-Qudra amesema utawala ghasibu wa Isarel unalenga hospitali kimakusudi,akisisitiza kwamba hatua hizo zinalenga "kuondoa" mfumo wa afya wa eneo la Palestina.

3486463

Habari zinazohusiana
Kishikizo: palestina gaza watoto
captcha