IQNA

Jinai za Israel

Wafadhili Qatar waanzisha kampeni ya kukusanya dola milioni 2.7 uisaidia Gaza

17:28 - August 16, 2022
Habari ID: 3475631
TEHRAN (IQNA) – Kampeni ya ‘Kujitolea kwa ajili ya Gaza’ imezinduliwa na Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Qatar.

Kampeni hiyo inalenga kukusanya QR10 milioni ($2.7m) kusaidia kujenga upya nyumba zilizoharibiwa wakati wa mashambulizi ya hivi majuzi ya siku tatu ya utawaladhalimu wa Israel dhidi ya Gaza.

"Maafa ya Gaza yanaendelea, pamoja na vita vya mara kwa mara na vikwazo vya miaka 15," alielezea Katibu Mkuu wa jumuiya, Balozi Ali Al-Hammadi.

"Kwa mara nyingine tena, majeshi ya Israel yameshambulia Gaza, na kusababisha Wapalestina huko kuppata maumivu na mateso zaidi."

Mashambulizi hayo ya anga yaliyoanza Agosti tano na kuendelea kwa siku tatu yaliharibu nyumba za raia, aliongeza.

"Wanaume, wanawake na watoto hawakuwa salama. Kwa kusikiliza sauti zao, jumuiya kwa niabaya watu wa  Qatar inanyoosha mkono wa kibinadamu ili kupunguza maumivu yao na kuwasaidia katika hali ngumu sana."

Kampeni hiyo itahakikisha usalama wa chakula, afya, maji na usafi wa mazingira pamoja na makazi.

"Lengo ni kupunguza athari za vita, kukuza ujasiri wa Gaza, na kuwezesha ahueni kutokana na masaibu haya."

Wakati wa uvamizi wa hivi punde wa Israel dhidi ya Gaza, Wapalestina 49, wakiwemo watoto wasiopungua kumi na saba na wanawake wanne waliuawa. Wengine 360 ​​walijeruhiwa.

3480106

Kishikizo: gaza ، qatar ، palestina ، israel ، jinai
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha