IQNA

Fikra za Kiislamu

Njia ya Kufikia Wokovu

23:30 - August 18, 2022
Habari ID: 3475644
TEHRAN (IQNA) - Mwanadamu daima yuko katika kutafuta furaha na wokovu na huwa anapouona wokovu huu katika viwango tofauti vya mtu binafsi, familia na kijamii.

Njia hii ya kutafuta wokovu wakati mwingine inachosha sana kwa mwanadamu kwani kuna haja ya kuwa na mtazamo wazi wa wokovu katika akili ya mtu kabla ya kuanza juhudi yoyote. Mtu hawezi kuelewa njia hii isipokuwa awe na mawazo yenye mantiki kuhusu wokovu.

Hatua ya kwanza ya kuweka mguu kwenye njia ya wokovu ni kuelewa fikra hii ya wokovu na nukta muhimu za kufanikisha safari hii.

Mwenyezi Mungu ameiweka wazi njia ya wokovu kwa wanadamu kupitia kwa Mtume Muhammad (SAW). "Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.” (Surah Al-Ahqaf, aya ya 9)

Kwa mujibu wa aya hii, Mtume (SAW) alikuwa na jukumu la kuongoza  umma kuelekea katika wokovu. Aya hiiinamuelezea kuwa ni mfuasi wa wahyi; ikimaanisha kuwa elimu ya Mtume moja kwa moja inatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni mjuzi wa kila kitu. Mtume Muhammad (SAW) anaelezea kufuata yale yaliyoteremshwa kuwani njia ya kufikia wokovu.

Wakati watu wanashikilia imani imara katika dini na kuhakikisha kwamba njia hii ndiyo kitu pekee kinachoweza kuwaokoa, basi wanapaswa kuweka uwezo wao wote kuikaribia njia hii.

Mtume Muhammad (SAW), alikuwa akitafuta kutimiza kazi ambazo Mwenyezi Mungu alimpa.

Mtume (Swalla Allaahu ´Alayhi wa Sallam) alikuwa akizingatia jinsi ya kutatua matatizo huku watu wengi wakitamani tu maisha yasiyo na matatizo. Kwa maneno mengine, Mtume Muhammad (SAW) alikuwa anafahamu vyema kwamba tutakumbana na changamoto katika maisha hivyo alijaribu kujifunza mbinu za kukabiliana na matatizo hayo.

Kwa hiyo, kuchukua njia ya wokovu kunahitaji kwamba tutambue njia hii kwanza na kisha tutende kulingana na maarifa tuliyopata.

Kishikizo: wokovu ، uislamu ، mtume muhammad saw
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha