IQNA

13:58 - May 15, 2022
Habari ID: 3475252
TEHRAN (IQNA)- Hayya Alal Falah ni sehemu ya Adhana au wito wa Sala katika Uislamu na maana yake ni Haya njooni kwenye kufaulu, mafanikio au wokovu.

Sasa swali hapa ni hili,  je ni vipi Sala itapelekea tufikie wokovu, mafanikio na ustawi.

Katika Qur'ani Tukufu neno 'Falah' limetajwa mara kadhaa. Kwa mfano Surah Al Muminun imeanza kwa aya isemayo: "Hakika amefanikiwa wamefanikiwa Waumini".

Katika aya ya 5 ya Surah al Baqarah tunasoma hivi: " Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa".

Halikadhalika katika Aya ya 64 ya Surah Taha, Allah SWT anasema: "Kwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha mfike kwa kujipanga safu, na kwa yakini atafuzu kweli kweli leo atakaye shinda."

Kila mtu anatafuta mafanikio, ufanisi na furaha katika maisha na ni nadra kumpata mwanadamu asiyetaka hayo. Ili kupata mafanikio, mwanadamu anapaswa kuvuka vizingiti na anapopata ufanisi na furaha, neno Falah linaweza kutumika kama mojawapo ya sifa alizonazo.

Lengo kuu la wokovu wa mwanadamu limo katika yeye kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na hilo linaweza kupatikana tu kwa kumtii Mwenyezi Mungu. Pamoja na hayo vishawishi vya kidunia humzuia mwandamu kujikurubishwa kwa Mola Muumba.

Kwa msingi huo,  Mwenyezi Mungu ametuandalia mazingira ya kufikia wokovu. Njia bora zaidi ambayo inaweza kutusaidia katika kuondoa vizingiti ni kumkumbuka Mwenyezi Mungu au dhikri na dhihirisho bora zaidi la dhikri ni katika Sala tano za kila siku zilizofaradhishwa kwa Waislamu.

Hivyo sala inaweza kutunusuru kutoka katika vishwawishi vya kidunia na minyororo ya shetani na kutuongoza katika maisha halisi ya mwanadmau ambayo ni maisha ya kuelekea katika ubora wa kimaanawi.

Sala ni aina bora zaidi ya Dhikri na humsaidia mwanadamu kustawi kimaanawi na kujiweka mbali na maovu.

Katika aya ya 45 ya Sura Al Ankabut, Allah SWT anasema:  SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda.

Pia katika aya ya 14 ya Sura Taha Allah SWT anamwambia Nabii Musa AS hivi:

"Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi."

*Makala hii imenukuliwa kutoka kitabu cha  "Kuelekea Kwako" cha Ayatullah Taqi Misbah Yazdi (1935-2021) , faqihi, mwanafalsafa, mfasiri wa Qur;ani na mmoja wa wanafikra waliobobea na mhadhiri katika vyuo vya kdini vya Qum nchini Iran.

Kishikizo: sala ، uislamu ، qurani tukufu ، misbah yazdi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: