Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika mji mtakatifu wa Qum Jumapili, Hujjatul Islam Mahdi Azizan, Rais wa Taasisi ya Utafiti wa Sayansi za Kiislamu ya Imam Sadiq (AS), ametoa kauli yake hiyo kuhusu muundo wa Akili Mnemba, akisisitiza athari zake za kifalsafa pamoja na vipengele vyake vya kisayansi.
Azizan anasema kwamba kosa la kawaida ni kutafsiri Akili Mnemba kwa mtazamo wa sayansi za kimaadili pekee.
Anasisitiza kwamba Akili Mnemba kwa asili ina maudhui au vipengee kadhaa, na kwamba ni daraja kati ya falsafa na sayansi za kimaadili. Kulingana na Azizan, "kipengele cha kifalsafa cha Akili Mnemba hakijapatiwa uzito wa kutosha."
Moja ya masuala muhimu ambayo Azizan anasisitiza ni ukosefu wa uwezo wa Akili Mnemba kujihusisha na fikra dhahania. Anasema kwamba, licha ya maendeleo ya kiteknolojia, AI haiwezi kufikia uwezo huu.
Akiangazia falsafa ya Kiislamu, anaeleza kwamba fikra za kibinadamu zina msingi wa fikraa dhahania na za kimataifa, ambazo si za kimashine na ni muhimu kwa kufikiri kwa kweli. Kinyume chake, Akili Mnemba inafanya kazi ndani ya muundo wa kimashine, ambao, kwa mujibu wa Azizan, "unazuia kuiga kikamilifu kazi za ufahamu wa kibinadamu."
Anasisitiza kwamba Akili Mnemba haina uwezo wa ubunifu na uvumbuzi, ambazo ni za asili katika fikra za binadamu. Aidha, akili ya kiroho, ambayo inajumuisha uwezo wa kuungana na kile kisichoonekana, ni pekee kwa wanadamu na inazidi uwezo wa mashine. "Hisia za binadamu kama furaha, huzuni, shangwe, na matumaini hakiwezi kuhamasishwa kwa mashine au Akili Mnemba.," anasema.
Nukta hii ya kihisia ni kipengele cha msingi cha uzoefu wa binadamu ambacho Akili Mnemba haiwezi kufikia.
Mwanazuoni huyo wa Kiislamu anasema Akili Mnemba ni "chombo cha thamani" lakini kamwe haitachukua nafasi ya fikra za kibinadamu. Aidha amesema kwamba teknolojia hii, kama ubongo wa kibinadamu, ni chombo kilichotumikia roho ya kibinadamu.
Halikadhalika Hujjatul Islam Mahdi Azizan amesema Akili Mnemba inaweza kuimarisha uwezo wa kibinadamu lakini haiwezi kuchukua nafasi ya sifa za kipekee za binaadamu kama viumbe wanaofikiri, wabunifu, kiroho, na kihisia. " Akili Mnemba haitawahi kuchukua nafasi ya wanadamu," anasisitiza.
4254470