IQNA

Fikra za Kiislamu

Siasa katika Uislamu hazina udanganyifu na hadaa

22:15 - August 27, 2022
Habari ID: 3475689
TEHRAN (IQNA) - Siasa katika Uislamu haimaanishi hila, hadaa na udanganyifu, badala yake dini hii tukufu inasisitiza maadili bora na uaminifu kuwa miongoni mwa vipengele vikuu katika siasa

Ufuatao ni mukhtasari wa hotuba iliyotolewa na Hujjatul Islam Nasser Rafiei, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa, kuhusu siasa katika Uislamu:

Dhana ya siasa katika Uislamu ni tofauti na ile iliyoanzishwa na nchi za Magharibi. Dini bila siasa si dini; kama alivyosema Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu-, mtu akitenganisha dini na siasa, haelewi dini wala siasa kwa usahihi.

Maimamu wote wa  Ahul Bayt au nyumba ya Mtume Muhammad SAW waliuawa shahidi kwa sababu walikuwa na misimamo kisiasa na walikuwa na waliwapinga  watawala katika kipindi chao. Lau wasingekuwa na mwelekeo wa kisiasa na iwapo walikuwa wanajishughulisha tu na ibada yao, hawangenyanyaswa na kuuawa shahidi na watawala dhalimu wa wakati wao.

Siasa za Magharibi ni sawa na udanganyifu na hila. Hii ni katika hali ambayo Imam Ali (AS) aliwahi kusema kutekeleza msamaha na uadilifu ni moja ya pambo la mwanasiasa. Baadhi ya fadhila zimefafanuliwa ipasavyo kwa mwanasiasa; kwanza kabisa, mwanasiasa anahitaji kuheshimu haki za Mwenyezi Mungu, walio hai, na wafu, kutii maagizo ya kidini, na kujiepusha na yale ambayo yamekatazwa na Mwenyezi Mungu.

Tunapaswa kuchunguza maisha ya Maimamu kwa ujumla wake, badala ya kuangazia sehemu ya maisha yao kwa malengo yetu ya kisiasa.

Utiifu kwa mtawala mwadilifu ni moja ya sifa nyingine za mwanasiasa. Hapa, kwa kuzingatia simulizi za Ahlul-Bayt (SA), mtawala mwadilifu na walii si lazima awe maasum au asiyetenda dhambi.

Sifa ya tatu ya mwanasiasa ni kuheshimu haki za wafu. Hatupaswi kuwakashifu na kuwatukana wafu, bali tunapaswa kuwasamehe na kuwaombea msamaha, isipokuwa watu kama Shimr na Yazid, ambao wanapaswa kulaaniwa daima.

3480234

captcha