IQNA

Fikra za Kiislamu

Qur'ani Tukufu inasemaje kuhusu kusafiri?

13:06 - August 21, 2022
Habari ID: 3475655
TEHRAN (IQNA) - Kusafiri sio tu kunaweza kuwa na faida za burudani lakini pia kuna jukumu kubwa katika kuboresha afya ya mtu kiakili. Ndio maana Qur'ani Tukufu ikapendekeza kusafiri na kujionea dunia.

Uislamu una mtazamo maalum na wa kina kuhusu kufanya safari. Kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu, pamoja na faida zake za nje, kusafiri kuna matokeo ya kiroho ambapo huboresha hali ya kiroho ya mwanadamu.

Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, safari ni fursa nzuri zaidi kwa mtu kuona yaliyobaki kutoka zamani na kutafakari juu ya maisha na ustaarabu wa wale walioishi zamani na waliyokuwa wakifurahishwa nayo katika muda wao mfupi wa kuishi duniani.

Qur’ani Tukufu inasema katika aya ya 21 ya Surah Al-Ghafir: “ Kwani hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Hao walikuwa wamewazidi hawa kwa nguvu na athari katika nchi. Na Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa kuwalinda na Mwenyezi Mung.”

Aya hii inarejelea majengo yenye nguvu ambayo wale walioishi kabla wamejenga. Jengo hili ambalo sasa si chochote ila magofu liliwahi kuwaweka watu ambao walidhani wangeishi maisha marefu au hata milele. Ndiyo maana walimsahau Mwenyezi Mungu na wakatumbukizwa katika dhambi na hatimaye waliadhibiwa au wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi na majengo yao yenye nguvu na vingine vyote walivyokuwa navyo havitaweza kuwaokoa.

Kwa hivyo, kwa kuzingatia Qur'ani, kusafiri kunapaswa kujumuisha kutazama kwa uangalifu na kutafakari juu ya maisha ya wale walioishi duniani hapo awali. Tafakari hii inapaswa kutufikisha kwenye hitimisho na kuamini kwamba sisi pia tutaondoka katika ulimwengu huu hivi karibuni na tutakuwa somo kwa vizazi vijavyo.

captcha