IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Kituo cha Kiislamu Uholanzi kimeharibiwa katika mashambulizi

22:07 - August 20, 2022
Habari ID: 3475652
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kiislamu huko Veldhoven kusini mwa Uholanzi kilishambuliwa mapema Jumamosi asubuhi katika kile kinachoonekana ni kitendo cha chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia.

Polisi wanachunguza shambulio hilo ambapo wahusika walivunja madirisha mawili na kuwasha moto jikoni..

Shambulio hilo lilitokea mapema usiku wa kuamkia Jumamosi. Watu kadhaa wanaoishi karibu waliwaambia polisi waliona mtu mmoja au wawili wakipanda juu ya lango la kituo hicho cha Kiislamu. Wakazi pia walisikia pikipiki ikiondoka wakati fulani usiku.

Wazima moto waliweza kuzima moto haraka, ambao uliacha uharibifu wa jikoni na maeneo mengine ya jengo hilo. Wapelelezi tayari wanakagua kamera za usalama katika eneo hilo ili kuwakamata wahalifu waliohusika na jinai hiyo.

Kituo cha Kiislamu, ambacho kilifunguliwa bila kutangazwa katika ukumbu wa zamani wa Judo mwezi Juni, kilizua mabishano miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

3480171

captcha