IQNA

Waislamu Ulaya

Eneo kubwa zaidi la makaburi ya Waislamu Ulaya Magharibi lazinduliwa Uholanzi

19:03 - January 14, 2023
Habari ID: 3476400
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Waislamu nchini Uholanzi imezindua makaburi makubwa zaidi ya Waislamu wa Ulaya Magharibi nchini Uholanzi.

Makaburi hayo yanayoitwa Maqbara Rawdah Al Muslimin (Bustani ya Makaburi ya Waislamu), yana nafasi ya kuzikwa miili 16,000. Kwa hiyo, ni makaburi makubwa zaidi ya Kiislamu katika eneo la Ulaya Magharibi.

Kulingana na Säid Bouharrou, mmoja wa waanzilishi wa mradi huo, Maqbara Rawdah Al Muslimin inakidhi mahitaji ya Waislamu nchini humo. Kwa vile makaburi mengi ya umma yana sera kwamba makaburi huvunjwa baada ya miongo kadhaa, Waislamu mara nyingi huchagua kuzikwa katika nchi yao ya asili. Lakini sasa kuna  kizazi kipya ambacho kimezaliwa Uholanzi na sasa huzikwa katika nchini humo.

Aidha wakati wa janga la corona, kulikuwa na  vizuizi vya kusafiri na hivyo Waislamu  wengi hawakuwa na budi ila kuzikwa kwenye makaburi ya umma hadi walipoweza kusafirishwa hadi nchi nyingine.

3482074

captcha