IQNA

Waislamu wa jamii ya Rohingya

Kifo cha taratibu cha Waislamu wa Rohingya

15:44 - August 24, 2022
Habari ID: 3475674
TEHRAN (IQNA) - Katika mwaka wa tano wa kulazimishwa kuhama Waislamu walio wachache wa Rohingya kutoka makwao nchini Myanmar, wengi wanaishi katika kambi ndani na nje ya nchi.

Jarida la Economist limeandika katika ripoti yake kuhusu hali ya Waislamu wa Rohingya: "Mauaji ya mwaka 2012 yalifungua njia ya umwagaji damu mkubwa zaidi, ambapo mwaka 2017, vikosi vya usalama vya Myanmar vilifanya mauaji ya umati, ubakaji na uchomaji moto katika eneo la Rakhine na matokeo yake watu wapatao 750 elfu wa jamii ya Rohingya walikimbilia Bangladesh; ambayo sasa imekuwa kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.

Ghasia katika kambi za Bangladesh dhidi ya Waislamu wa Rohingya

Gazeti hilo linasema kwamba kwenda Bangladesh ilikuwa rahisi kidogo mwanzoni. Lakini serikali ya Bangladesh hatua kwa hatua iliwatazama wakimbizi kama mzigo mabegani mwake, na vurugu zikaenea katika kambi hizo; Ghasia nyingi zilifanywa na vikosi vya usalama vya serikali.

The Economist limeongeza kuwa: "Leo, karibu theluthi moja ya Warohingya walio wachache waliosalia nchini Myanmar wanaishi katika kile ambacho kundi la shinikizo la Fortify Rights linakiita "kambi za kizuizini za kisasa"; Hapo awali kambi hizo ziliundwa kudumu kwa miaka miwili pekee na nyingi zimeathiriwa vibaya na mafuriko katika muongo mmoja uliopita."

Umoja wa Mataifa unasema hali hiyo inaonekana kuwa kifo cha polepole kwa Warohingya; Kwa sababu idadi yao imepungua sana nchini Myanmar.

The Economist inaamini kuwa maadamu jeshi la Myanmar liko madarakani, ni vigumu kubadilika hali ya Warohingya.

Mohammad, ambaye ni mmoja wa wakazi wa kambi hiyo, anasema: "Maisha katika kambi ni mabaya zaidi kuliko jela. Kwa sababu wafungwa wanajua muda wa chini kabisa wa kifungo chao. Lakini Warohingya hawajui kama wataachiliwa au la. Hata wakiachiliwa, wengi wao hawana nyumba ya kurudi. Kwa sababu polisi waliharibu magofu ya nyumba zao kwa tingatinga na kuuza ardhi."

captcha