IQNA

Jinai za Myamar

Ushahidi kuhusu namna Jeshi la Myanmar lilivyopanga kuwaangamiza Waislamu

21:03 - August 05, 2022
Habari ID: 3475583
TEHRAN (IQNA) – Nyaraka mpya zinaonyesha jinsi vikosi vya jeshi la Myanmar vilipanga kuwafukuza kwa lazima Waislamu walio wachache wa nchi hiyo kutoka ardhi zao za jadi.

Wachunguzi wa uhalifu wa kivita wamepata maelfu ya nyaraka zinazotoa mwanga mpya kuhusu mpango wa jeshi la Myanmar kuhusu kuwatimua kwa nguvu Waislamu walio wachache katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia kutoka katika ardhi zao za jimbo la Rakhine.

Nyaraka hizo ni sehemu ya idadi kubwa ya nyaraka, zilizokusanywa na wachunguzi wa uhalifu wa kivita zinazofichua mipango ya kuangamiza watu wa Rohingya.

Kwa muda wa miaka minne iliyopita, wachunguzi hao wamekuwa wakifanya kazi kwa siri kukusanya ushahidi wanaotumai unaweza kutumika kuwatia hatiani maafisa wa kijeshi wa Myanmar katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Kundi lililokusanya nyaraka hizo tayari limezifikishwa kwa waendesha mashtaka huko The Hague.

Kuanzia mwaka wa 2018, Tume ya Haki ya Kimataifa na Uwajibikaji (CIJA), shirika lisilo la faida linalofanya kazi na mawakili wa kimataifa wa uhalifu ambao wamefanya kazi Bosnia, Rwanda na Kambodia, ilikusanya kurasa 25,000 za hati rasmi, nyingi zinazohusiana na kufukuzwa kwa jamii ya Waislamu Rohingya. .

Nyaraka hizo zinaonyesha namna watawala wa Myanmar walivyokuwa na chuki ambayo iliwapelekea wasisitize kupunguza idadi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ambayo waliiona kama tishio kwa uwepo wa Myanmar.

Katika mkutano wa faragha na maafisa wa Rakhine, ambao ulifanyika wakati wa kufukuzwa Waislamu mwaka 2017, mkuu wa jeshi wakati huo na kiongozi wa sasa wa utawala wa kijeshi, Min Aung Hlaing, aliwaambia Wabudha wabakie katika eneo hilo na wasihame huku akaashiria kukosekana kwa usawa wa idadi ya watu ambapo Warohingya walionekana kuwa wengi zaidi ya jamii zingine jimboni Rakhine, nyaraka zinaonyesha.

Makamanda wakuu wa jeshi la Myanmar baadaye walijadili njia za kuingiza majasusi katika vijiji vya Rohingya kubomoa nyumba na misikiti ya Waislamu.

Majadiliano  hayo ya kuwatimuwa Waislamu yamenaswa katika rekodi rasmi.

Katika mkutano mmoja, makamanda walitumia mara kwa mara maneno ya ubaguzi wa rangi kwa Warohingya wakiwataka kuwa ni raia kigeni walioingia nchini humo.

Makamanda walikubali kuratibu mawasiliano kwa uangalifu ili jeshi kuingia na kutekeleza oparesheni za kuwatimua Waislamu "papo hapo na kwa wakati."

Kufikia katikati ya Agosti 2017, mamia ya wanajeshi walikuwa wamesafirishwa hadi kaskazini mwa Rakhine.

Wiki kadhaa baadaye, jeshi la Myanmar lilianza ukandamizaji wa kikatili ambao ulipelekea takriban Warohingya 800,000 kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh.

Kiongozi wa kiraia wa Myanmar wakati huo, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Aung San Suu Kyi alipuuzilia mbali ukosoaji mwingi wa jeshi. Lakini nyaraka rasmi za kipindi cha kabla na wakati wa kufukuzwa kwa Warohingya zinatoa picha tofauti.

Nyaraka hizo zinaonyesha jinsi wanajeshi walivyoeneza chuki dhidi Waislamu walio wachache, wakaunda wanamgambo ambao hatimaye walishiriki katika operesheni dhidi ya Warohingya, na  vitendo hivyo vya jinai dhidi ya Waislamu viliratibiwa watawa wa Kibudha wenye imani kali sana.

Tukio la mauaji ya kinyama la Agosti 2017 lilitekelezwa kwa ukatili ambao ulishangaza ulimwengu. Wakimbizi walielezea mauaji, ubakaji wa magenge na watoto kutupwa kwenye moto mkali.

Mapema Agosti 25, polisi zaidi 22 vilishambuliwa na wanaume wa Rohingya kaskazini mwa jimbo la Rakhine, na kuua askari 12, mamlaka ilisema.

Wanaume hao kwa kiasi kikubwa hawakuwa na mafunzo na walikuwa wamebeba fimbo, visu na mabomu ya kutengenezewa kienyeji, kulingana na UN.

Baadhi ya askari wa vikosi vya usalama walisema wameshangazwa na majibu yasiyolingana ya jeshi hilo kwa kile walichosema kuwa ni mashambulizi yaliyopangwa vibaya ikilinganishwa na uasi unaofanywa na wanamgambo wenye vifaa vya kutosha katika maeneo mengine ya nchi.

Asubuhi iliyofuata, kuchomwa moto kwa vijiji vya a Waislamu wa jamii yRohingya kulianza. Ripoti zinaelezea "mashambulizi ya uchomaji moto" katika kitongoji cha Rakhine cha Maungdaw, ambapo nyumba, maduka, misikiti na shule ziliharibiwa au kuteketezwa

Uchomaji moto uliendelea kwa wiki. Zaidi ya makazi au majengo 7,000 yalihabomolewa na kuteketezwa moto kati ya Agosti 25 na katikati ya Septemba.

Moe Yan Naing, inspeckta  polisi ambaye aliwekwa katika eneo la cha Rakhine, alisema wakuu wake walimwamuru yeye na wenzake kuchoma moto vijiji. Kulikuwa na maiti nyingi katika vijiji.

"Wanajeshi walipiga risasi katika kijiji kabla ya kuingia," alisema, akimaanisha kijiji cha Inn Din, ambapo vyombo vya habari vilifichua mauaji ya raia. "Walimpiga risasi na kumuua yeyote waliyemkuta kijijini."

Zaidi ya vijiji 390 viliharibiwa kwa sehemu au kabisa, kwa kiasi kikubwa kwa moto. Hii ilifikia 40% ya vijiji vyote kaskazini mwa jimbo la Rakhine.

Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) wanasema inakadiriwa kuwa takriban Waislamu 10,000 waliuawa huku mamia ya vijiji vya Waislamu wa Rohingya viliteketezwa kwa moto.

Mapema mwaka jana, jeshi liliipindua serikali ya Suu Kyi, ambaye amekuwa akizuiliwa tangu kupinduliwa kwake. Mapinduzi yamebadilisha maoni nchini Myanmar na kupelekea kuanza uchunguzi wa jinai dhidi ya Waislamu.

Wakati jeshi la Myanmar linakabiliwa na tuhuma nzito chini ya sheria za kimataifa, bado njia ya kuwafikisha kizimbani ni ndefu.

Myanmar haijatia saini Mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambayo ina uwezo wa kuwahukumu wahusika katika nchi ambao wamepatikana na uhatia ya jinai za kivita.

Lakini njia zingine za kuanzisha kesi. Mahakama ya ICC iliweka mfano wa kisheria mwaka 2019 kwa kuruhusu mwendesha mashtaka wake mkuu kuanza kuchunguza uhalifu dhidi ya wakazi wa Rohingya, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza nchini, kwa sababu walikimbilia Bangladesh, ambayo ni mwanachama wa mahakama.

Mnamo mwaka wa 2019, Gambia yenye Waislamu wengi iliwasilisha kesi mauaji ya halaiki dhidi ya Myanmar katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), kwa niaba ya nchi 57 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu. Mnamo Julai, mahakama iliidhinisha kesi hiyo kuendelea, ikikataa pingamizi lililowasilishwa na Myanmar.

Chombo cha Umoja wa Mataifa pia kimekuwa kikikusanya ushahidi kuhusu jinai za kjeshi la Myanmar huko Rakhine.

3479983

Kishikizo: rohingya ، jinai ، waislamu ، myanmar
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha