IQNA

Ubaguzi wa rangi

Ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya Waislamu wenye asili ya Afrika

12:25 - August 25, 2022
Habari ID: 3475677
TEHRAN (IQNA)- Utafiti wa Chuo Kikuu cha Rice unaonyesha kuwa Waislamu wenye asili ya Afrika nchini Marekani wanakabiliwa na utumiaji mabavu na unyanyasaji mara tano zaidi yaw engine kutoka kwa polisi nchini humo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Rice, Waislamu kutoka Mashariki ya Kati au Afrika wana uwezekano mkubwa wa kunyanyaswa na polisi kwa sababu ya dini yao kuliko Waislamu wazungu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa Waislamu wa Marekani wana uwezekano mara tano zaidi wa kunyanyaswa na polisi, lakini Waislamu wazungu wana uwezekano mdogo wa kunyanyaswa na polisi.

Uchunguzi unaonyesha kwamba uhusiano kati ya jumuiya za Kiislamu na polisi wa Marekani umekuwa si mzuri, na Waislamu wengi hawana imani na polisi kwa sababu ya sera za baada ya mashambulio ya 9/11.  Utafiti wa Chuo Kikuu cha Rice pia unaonyesha kwamba Waislamu wengi wa Marekani wanaogopa kutokana na kufuatiliwa na polisi kupitia hatua kama vile ufuatiliaji mtandaoni, viwanja vya ndege, vituo vya kawaida au ufuatiliaji wa maeneo ya kidini.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa zaidi ya 23% ya Waislamu wenye asili ya Afrika  wamekumbana na unyanyasaji wa polisi. Ripoti ya Taasisi ya Pew pia inaonyesha ongezeko la kutisha la ubaguzi wa rangi, kikabila na kiitikadi nchini Amerika.

Utafiti mpya uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Pew katika nchi 17 unaonyesha kuwa wasiwasi juu ya ubaguzi wa rangi na kikabila nchini Marekani ni mbaya.

Kulingana na Raw Story, ripoti ya Taasisi ya Pew iligundua kuwa wastani wa asilimia 89 ya watu 16 wasio Waamerika wanaelezea ubaguzi wa rangi na kikabila nchini Marekani kama "tatizo fulani" au "zito sana".

Katika utafiti huu uliofanywa katika nchi za Marekani, New Zealand, Ujerumani, Korea Kusini, Kanada, Japan, Uholanzi, Uhispania na Uswidi, vijana wanaona ubaguzi ni tatizo zaidi kuliko watu wazima na wanawake kuliko wanaume.

Kwa mfano, asilimia 80 ya wanawake wanasema ubaguzi kulingana na rangi au kabila ni "tatizo fulani" au "zito sana". Idadi hii ni 68% kwa wanaume.

Pia, ubaguzi wa kijinsia unaonekana nchini Kanada na Ujerumani kwa takriban 10%.

4080607

captcha