IQNA

Waislamu Kanada

Waislamu wakosoa uamuzi wa kuondoa bango lenye Hijabu huko Montreal

22:16 - November 01, 2024
Habari ID: 3479680
IQNA – Mji wa Montreal utatuma ujumbe usio sahihi ikiwa utatoa bango kukaribisha katika ukumbi wa jiji ambalo linajumuisha mwanamke aliyevaa Hijabu. Haya ni kwa mujibu wa kundi la kitaifa la kutetea Waislamu wa Kanada.

Haya ni kwa mujibu wa kundi la kitaifa la kutetea Waislamu wa Kanada.
Stephen Brown, mtendaji mkuu wa Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Kanada, alisema Jumatano shirika lake lilishangazwa na kukatishwa tamaa na uamuzi wa jiji hilo.
Meya wa Montreal Valérie Plante aliambia kipindi cha mazungumzo cha televisheni ambacho kilirushwa hewani siku ya Jumapili kwamba mchoro unaoonyesha mwanamke aliyevaa Hijabu utaondolewa ili kukidhi matakwa ya kutoegemea dini, akiongeza kuwa picha ya mwanamke mwenye Hijabu liliwafanya baadhi ya waingiwe na wasiwasi.
Picha, iliyochorwa kwa penseli, inaonyesha mwanamke mwenye Hijab akiwa amesimama kati ya wanaume wawili - kijana mdogo amevaa kofia ya besiboli na mtu mzee aliyekunja mikono- ikiwa naa maneno "Karibu kwenye Ukumbi wa Jiji la Montreal!" kwa Kifaransa.
"Bango hili linawakilisha watu wa Montreal – sio nembo ya dini au wasiokuwa na dini," Brown alisema, akiongeza kuwa jiji lilipaswa kumwambia mtu yeyote ambaye alikuwa na wasiwasi kutembea katka jiji ajionee wanaoishi hapo.
"Nchini Kanada katika karne ya 21, hatuwaondoi watu kutoka kwa jamii kwa sababu ya jinsi wanavyoonekana," Brown alisema. "Bango hilo lilikuwa mwakilishi wa wenyeji wa Montreal na mtu yeyote anayetoka nje na kuzunguka Montreal kwa nusu saa ataona kila aina ya watu."

Kishikizo: kanada waislamu hijabu
captcha