IQNA

Qur’ani Tukufu Inakabiliana na Ubaguzi wa Rangi/3

Jinsi ubaguzi wa rangi unavyodhoofisha dini

18:46 - December 30, 2023
Habari ID: 3478115
IQNA – Watu hupotosha na kughushi ukweli kwa sababu tofauti, mojawapo ikiwa ni ubaguzi wa rangi na ukabila.

Tawi moja la ubaguzi wa rangi ni utaifa katika hali yake ya itikadi kali. Wabaguzi wa rangi na wenye utaifa wa itikadi kali  wakati mwingine hulazimisha maoni yao juu ya Uislamu na kusababisha upotoshaji wa fikra za Kiislamu. Kwa mfano, baadhi ya wanataifa wanadai kuwa Uislamu ni dhihirisho la utaifa wa Kiarabu.

Hata walighushi Hadith baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (SAW) ili kuendeleza mtazamo huo potovu.

Mfano mwingine ni Wayahudi ambao walipotosha ukweli ili kuthibitisha ubora wao juu ya wengine. Baada ya Musa (AS), kwa karne nyingi wanazuoni wa Kiyahudi waliipotosha Torati kulingana na matakwa yao ya kudumisha ushawishi na nguvu zao.

Kwa mujibu wa mwanafikra, neno Tahreef (upotoshaji) limetumika katika Qur'ani Tukufu hasa kuhusu Mayahudi ambao ni mabingwa wa upotoshaji sio tu leo bali tangu mwanzo.

Ilikuwa ni desturi kwamba wanachuoni wa Kiyahudi wangelipwa na Mayahudi ili kuwaambia kuhusu sifa za mjumbe wa mwisho wa Mungu (Mtume Muhammad (SAW).

Hata hivyo, Muhammad (SAW) alipoteuliwa kuwa mtume na wakatambua kuwa yeye ndiye Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, waliogopa kwamba kama watasema ukweli, Mayahudi wangeanza kusilimu na wanazuoni watapoteza pesa walizopokea kila mwaka. Basi wakaipotosha Taurati na wakabadilisha tabia zilizotajwa juu ya Mtume wa mwisho, hivyo wakawapoteza Mayahudi.

Katika Quran Tukufu, Mwenyezi Mungu anaidhihirisha sifa hii ya Wayahudi:

“Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangeli sema: Tumesikia na tumet'ii, na usikie na "Undhurna" (Utuangalie), ingeli kuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu." (Aya ya 46 ya Surat An-Nisaa)

captcha