IQNA

Kususia Israel

Tunisia yakanusha uhusiano wa kibiashara na utawala wa Israel

22:45 - August 25, 2022
Habari ID: 3475681
TEHRAN-(IQNA) - Wizara ya Biashara na Mauzo ya Nje ya Tunisia imekanusha ripoti zilizochapishwa kuhusu kuwepo kwa mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hii na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Nje ya Tunisia, huku ikikanusha mabadilishano yoyote ya kibiashara na utawala wa Kizayuni, ilisisitiza kuzingaitia kanuni ya kuisusia Israel ya nchi za Kiarabu.

Wizara hii ilisisitiza katika taarifa rasmi: “Tunisia imejiunga na Makubaliano ya Ushuru na Biashara (GATT) tangu mwaka 1990 na inatenda kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 35 ya mkataba huu kuelekea utawala wa Kizayuni.”

Wizara hii imesisitiza kuwa: Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, maingiliano yoyote na makampuni ya usafiri wa kigeni ambayo yatathibitika kukiuka kanuni na masharti yanayohusiana na vikwazo dhidi ya utawala wa Kizayuni wa nchi za Kiarabu ni marufuku. .

Hapo awali, tovuti ya "Com Trade" ilitangaza katika ripoti kwamba kiasi cha biashara kati ya Tunisia na Israeli ni dola milioni 29.

Kulingana na tovuti hii, Tunisia inaagiza vifaa vya kielektroniki, mafuta ya wanyama na mboga, saa na vifaa vya matibabu kutoka Israel, na kinyume na Israel, inaagiza nguo na vyakula kutoka Tunisia.

Hapo awali, Mohamed Ali Al Farshishi, msemaji wa Wizara ya Biashara ya Tunisia, alikanusha kuwepo kwa mabadilishano yoyote rasmi ya kibiashara kati ya Tunisia na Israel na kueleza: Mshirika wa kwanza wa Tunisia ni Umoja wa Ulaya, hivyo mshirika huyu anaweza kuuza bidhaa za Tunisia kwa Israel na Tunisia haiwajibiki na suala hilo.

4080594

captcha