Alaa Ghram anacheza kama mlinzi wa kati wa Klabu ya Ligi Kuu ya Ukraine, Shakhtar Donetsk, na timu ya taifa ya Tunisia.
Picha za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akisoma Qur'ani ziliwekwa kwenye ukurasa rasmi wa timu ya Ukraine kwenye Facebook.
Alipigwa picha wakati wa safari ya timu kwenda London kumenyana na Arsenal katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA.
Chapisho hilo lilipata zaidi ya likes 20,000 kwa muda mfupi, kulingana na tovuti ya Bayan-gate.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii walimsifu Ghram kwa kuzingatia mambo ya kiroho kabla ya mechi muhimu dhidi ya Arsenal.
4243707