IQNA

Umoja wa Kiislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Maadui wanataka kuleta mgawanyiko baina ya Waislamu

8:30 - September 03, 2022
Habari ID: 3475724
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria majaribio ya maadui ya kutaka kuleta mgawanyiko baina ya Waislamu na kuwasilisha taswira potovu ya kuuonyesha Uislamu kuwa ni dini ya ghasia na mapigano na kusema kuna haja ya kutilia mkazo juu ya umoja wa makundi ya Kiislamu na juhudi za kuutambulisha Uislamu wa kweli.

Akizungumza katika kikao na wajumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt kutoka nchi 118 kinachofanyika mjini Tehran, Hossein Amir-Abdollahian alizungumzia hali iliyopo ya ulimwengu wa Kiislamu na vitisho na fursa zilizo mbele yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuundwa kwa makubaliano ya kimataifa dhidi ya ghasia, kwa kuzingatia mafundisho ya Kiislamu kuhusu amani na uadilifu na kufichuliwa kwa vipengele vinavyokinzana vya haki za binadamu za Magharibi.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake amesema mazungumzo na utendaji wa Jamhuri ya Kiislamu katika siasa za nje umejengeka katika msingi wa uhuru na kujitegemea, amani na heshima.

Waziri Amir-Abdollahian alitaja maandalizi ya mazingira ya kubadilishana mawazo wanazuoni wa Kiislamu duniani kuwa ni moja ya mafanikio yenye thamani ya Mkutano Mkuu wa 7 Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt .

Kongamano la Saba la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlu Bayt (AS) mjini Tehran lilianza Alhamisi kwa hotuba ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na linatazamiwa kumalizika leo.

Kongamano hilo linajadili masuala ya vyombo vya habari, intaneti, familia, wanawake katika vyuo vikuu na uchumi. 

3480314

captcha