IQNA

Umoja wa Kiislamu

Rais Raisi wa Iran asema Ahlul Bayt AS ni siri ya Umoja wa Kiislamu

14:47 - September 01, 2022
Habari ID: 3475717
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ahlul Bayt AS- yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW, ni ufungu wa Umoja wa Kiislamu na chimbuko la matumaini katika jamii ya mwanadamu.

Rais Sayyid Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo alipohutubu katika Kongamano la Saba wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS leo mjini Tehran.

Rais wa Iran amebaini kuwa leo mwanadamu amepoteza uadilifu na kuongeza kuwa, Ahlul Bayt AS ni siri ya kupigania uadilifu  duniani. Ameendelea kusema kuwa: "Uadilifu ni kitu kilichojikita katika nafsi na asili ya wanadamu wote."

Raisi amesema: "Ulimwengu unazingatia kwa njia maalumu fikra za Ahlu Bayt kwani fikra hii ni ya haki na uadilifu, ubinaddamu na mantiki kamili."

Rais wa Iran amesema vijana hasa katika nchi za Magharibi wanaelekea kwa wingi katika dini na umaanawi na kadhiaa hii inamaanisha kuwa wanaozuoni waliokusanyika katika kongamano wana jukumu kubwa.

Aidha rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ahlu Bayt AS ndio ufungua wa wema na ni nembo ya mema mbali na kuwa dhihirisho la ubora wa dunia sambamba na kuwa ufunguo wa sayansi, elimu, maadili, haki na umaanawi wa wanadamu.

Kwingineko katika hotuba yake, Raisi amesema uhusiano wa kielimu, kiutamaduni na kijami baina ya wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlu Bayt AS unaweza kuibua mustakabali mwema na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuratibu uhusiano huo.

Rais wa Iran amesema njia bora ya kuokoa taifa na mwanadamu wa sasa ni kuwajua Ahul Bayt AS na kuongeza kuwa: "Ahul Bayt AS ni ufunguo wa mema na ni dhihirisho la ubora wa dunia". Amesema Maimamu watoharifu katika maisha yao walijitahidi kuongoza wanadamu, kupambana na udhalimu na kuelimisha wanadamu."

Rais Ebrahim Raisi pia amesema wanazuoni wa Kiislamu wana jukumu kubwa la kuwaarifisha Maimamu  na viongozi wa wengine wa kidini na kuongeza kuwa: "Jukumu la wanazuoni ni kuhakikisha kuwa maneno ya Maimamu yanafahamika ili kuokoa jamii ya mwanadamu." Amesmea iwapo kutakuwa na uufahamu sahihi wa Ahlu Bayt AS, basi itaweza kubainika wazi kuwa kile ambacho mwanadamu wa sasa anakosa ni ufahamu sahihi kuhusu Imam Ali AS, Fatima Zahra AS na Imam Hussein AS. 

Kongamano la Saba wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlu Bayt AS litajadili masauala ya vyombo vya habari, itaneti, familia, wanawake na uchumi. 

4082476

captcha