IQNA

Umoja wa Waislamu

Shekhe Mkuu al-Azhar atoa mwito wa Umoja wa Kiislamu, mazungumzo Shia na Sunni

6:12 - November 05, 2022
Habari ID: 3476037
TEHRAN (IQNA)- Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri ametoa mwito wa Umoja wa Kiislamu sambamba na kufanyika mazungumzo baina ya Maulamaa wa madhehebu ya Shia na Sunni kwa ajili ya kukabiliana na fitina na mapigano ya kikaumu.

Sheikh Ahmad al Tayyib Shekhe Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amesema hayo katika hafla ya kufunga mkutano wa mazungumzo ya dini mbalimbali huuko nchini Bahrain na kubainisha kwamba, kuna haja ya kuweko mazungumzo ya Waislamu kwa Waislamu kwa kuhudhuriwa na Maulamaa wa Kishia na Kisuni.

Shekhe Mkuu wa Al-Azhar amesema: "Ninawatolea mwito Maulamaa wa Kiislamu ulimwenguni kote kuweka kando hitilafu zao za kimadhehebu na kufanya hima haraka ya kukutana katika mazungumzo ya kweli ya Waislamu kwa Waislamu katika kalibu ya umoja na kukurubisha pamoja fikra na kufahamiana zaidi." 

Ameendelea kusema kuwa:" Mimi binafsi na wanazuoni wakubwa wa Al Azhar pamoja na Jopo la Wazee wa Kiislamu tuko tayari kukaa katika meza ya duara na ndugu zetu wa Kishia na kuweka kando tofauti zeti ili kuimarisha Umohja wa Kiislamu."

Mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kisuni ameongeza kuwa, lengo la kikao hicho liwe ni kusahau yaliyopita na badala yake kuimarisha nguvu ya Uislamu sambamba na kuleta pamoja mitazamo na misimamo ya Kiislamu bila kusahau kuweka kando hotuba za chuki, uchochezi na ukufurishaji.

"Natoa wito kwa ndugu zangu na Maulamaa wa Kiislamu kote duniani wanafuata madhehebu zote kushiriki katika kikao cha mazungumzo ya Kiislamu," Sheikh al Tayyib alisisisitiza.

Kikao hicho cha Bahrain pia kimehudhuriwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ambaye anatembelea Ghuba ya Uajemi kwa mara ya kwanza kabisa.

 3481120

captcha