IQNA

Qur'an Tukufu Inasemaje/28

Kujisalimisha mbele ya ukweli hupelekea kuondoka hitilafu

16:22 - September 08, 2022
Habari ID: 3475753
TEHRAN (IQNA) – Dini ambazo wafuasi wake wana imani ya Mwenyezi Mungu zina mambo mengi yanayofanana katika misingi lakini pia dini hizi zina tofauti au hitilafu.

Kumekuwa na mawazo tofauti kuhusu hifilafu hizi ambazo wakati mwingine ni za upendeleo na wakati mwingine za haki na usawa. Lakini ni ipi njia ya msingi ya kuunda umoja na maelewano kati ya wafuasi wa imani mbali mbali?

Kuna aya katika Qur'ani Tukufu ambayo inaweza kutusaidia kufikia suluhu na ikieleweka vyema na kuifanyia kazi inaweza kuondoa tofauti zote:

“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” (Surah Al-Imran, Aya ya 19)

Neno Uislamu katika aya hii linaweza kuonekana kuwa na maana iliyo wazi lakini linaweza kutumika kuleta maana nne:

1. Yeyote anayekubali wahyi wa Mwenyezi Mungu ni mfuasi wa Uislamu. Kwa maneno mengine, Mwislamu ni mtu anayekubali dini ya Mwenyezi Mungu kwa akili yake na hiari yake.

2. Neno Muislamu linamaanisha kila kitu ambacho ulimwengu unakubali sheria za Mwenyezi Mungu. Ndiyo kusema viumbe vyote vinafuata sheria za asili na vinalazimika kutii matakwa ya kimungu kwa sababu vyote vimeumbwa na Mungu na hawana chaguo lingine zaidi ya kutii sheria za kimungu. Kwa mfano, jiwe halina chaguo lingine isipokuwa kuanguka chini kama matokeo ya mvuto, ambayo ni udhihirisho wa mapenzi ya Mungu katika ulimwengu wa nyenzo.

3. Muislamu pia ana maana tukufu inayowahusu watu watukufu wa Mungu. Kila sekunde ya maisha ya watu hawa ni kwa mujibu wa sheria ya Mungu.

4. Maana mahususi zaidi ya Uislamu inarejelea dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu ambayo ilifikishwa kwa wanadamu na Mtukufu Mtume (SAW) karne 14 zilizopita.

Kwa hiyo Uislamu ni ukweli wa jumla unaojumuisha wanadamu na mazingira na sababu kwa nini dini ya mwisho inaitwa Uislamu ni kwa sababu katika dini hii, mwanadamu anajisalimisha kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi.

Katika ufafanuzi wake katika Tafisri ya Nur ya Qur'ani Tukufu, Hujjatul Islam Muhsin Qara’ati anaashiria jumbe zifuatazo kutoka kwenye aya hii ya Qur'ani Tukufu

  1. Imani juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu, uadilifu, na hekima (iliyoonyeshwa katika aya iliyotangulia) huandaa njia ya kunyenyekea.
  2. Sharti la kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu ni kuukubali Uislamu kuwa ndio imani ya mwisho ya Mwenyezi Mungu (Dini pekee kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu).
  3. Kuvunja mipaka ya haki kunaleta tofauti: “…Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi…”
  4. Asili ya tofauti nyingi za kidini ni husuda na kutokujua ukweli.
  5. Wivu unaweka msingi wa Kufr (kufuru).
  6. Kitabu na elimu peke yake haviwezi kuwaokoa wanadamu.
  7. Wale wanaoleta tofauti na mifarakano watapata adhabu hivi karibuni.

3480338

captcha