IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /31

Sura Luqman: Ushauri wa Baba Mwenye Hekima kwa Mwanawe

16:29 - September 19, 2022
Habari ID: 3475809
TEHRAN (IQNA) – Luqman alikuwa mtu mashuhuri aliyeishi wakati wa Nabii Daud (AS). Alikuwa Hakim (mtu mwenye hekima) na kwa mujibu wa baadhi ya maelezo ya kihistoria alikuwa mtume wa Mwenyezi Mungu.

Sura Luqman katika Qur'ani Tukufu, inaashiria baadhi ya ushauri wake kwa mwanawe. Sura Luqman ni Sura ya 31 ya Quran. Ina Aya 34 na imo katika Juz 21 ya Kitabu kitukufu. Ni sura ya 57 ya Qur'ani iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Jina la Sura ni Luqman kwani inataja jina la bwana huyu mwenye hekima mara mbili. Ni sura pekee ya Qur'ani inayozungumza juu yake.

Kuna maoni tofauti kuhusu mahali alipozaliwa na muda gani aliishi. Lakini anajulikana kuwa muumini wa kweli, mkweli, na aliyesaidia watu kutatua tofauti zao.

Katika Sura hii, Luqman anamusia mwanawe kuhusu umuhimu wa kuwa na imani thabiti ya Tauhidi, kuwaheshimu na kuwatii wazazi, kuswali, kuendeleza wema na kuzuia maovu, kuwa na subira, kunyenyekea, kujiepusha na kiburi, na kuzungumza kwa busara.

Sura hii inawagawanya wanadamu katika makundi mawili: Waumini na watenda mema ni kundi la kwanza, na la pili ni la wapotovu na wenye kiburi. Katika baadhi ya aya ilieleza sifa na dalili zao na wapi wataishia katika dunia hii na ijayo.

Sura pia inazungumzia dalili za Tauhidi ukuu wa Mungu, na sababu zinazothibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.

Sehemu ya Sura Luqman ilieleza baadhi ya vipengele vya Siku ya Hukumu na jinsi mwanadamu katika ulimwengu huu wa mpito anavyoghafilika na yale yatakayokuja huko akhera.

Katika sehemu ya mwisho ya Sura, yametajwa masuala matano ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anajua: Siku ya qiyama itakapokuwa, kunyesha kwa mvua na ni matone mangapi ndani yake na athari zake, nini kiko matumboni mwa akina mama, hatima ambayo inawangoja watu, na jinsi gani na lini mtu atakufa.

Habari zinazohusiana
captcha