IQNA

Fikra za Kiislamu

Muongozo wa Qur'ani Tukufu kuhusu kudhibiti hasira

22:28 - September 18, 2022
Habari ID: 3475805
TEHRAN (IQNA) – Wanadamu wana hisia tofauti, ambazo baadhi zinaweza kusababisha tabia isiyofaa ambayo inahitaji kudhibitiwa ili isimzuie mtu kufikia malengo yake halali na ya juu..

Hasira ni kati ya mambo ambayo yanaweza kumuathiri kila mwanadamu. Lakini tusiiruhusu itawale tabia zetu kwa sababu la sivyo maisha na mahusiano yetu na wengine yatadhurika.

Kuna matukio mengi ambayo watu wamesababisha misiba kutokana na hasira zao na kujiingiza wenyewe na wengine katika hali ambazo matokeo yake hayawezi kufidiwa.

Hasira inaweza kuchukuliwa kuwa hali isiyo ya kawaida. Wanasaikolojia wanaamini kwamba ingawa hasira ni hisia mbaya na hasi, ni kama maumivu au joto la juu ambalo hutupatia onyo kuhusu jambo litakalotokea au mabadiliko yanayohitaji kufanywa.

Mafundisho ya Uislamu yanasema wanadamu bora ni wale ambao hawakasiriki kirahisi. Kwa mujibu wa Quran Tukufu, kuzuia hasira ya mtu ni njia mojawapo ya kupata msamaha wa Mungu:

“Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema."  (Surah Al Imran, Aya ya 133-134)

Kila mtu ana malengo katika maisha yake na kufikia mahitaji hayo kuna haja ya kwa na utulivu wa ndani na amani. Hasira ni kikwazo kikubwa kwa hilo. Idadi kubwa ya fursa hupotea kwa sababu ya hasira na ghadhabu. Ndio maana ushauri muhimu kutoka kwa Uislamu ni kutulia na kukataa kukasirika.

Waumini ni nadra kukasirika kwa sababu wanaboresha hali yao ya kiroho kwa kutekeleza majukumu ya kidini. Na wana njia bora zaidi ya amani ya akili:

 “Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua! .” (Surah Ar-Raad, Verse 28).

Kwa hivyo dhikri au kumkumbuka Mwenyezi Mungu mara kwa mara huleta utulivu moyoni na kuzuia hasira na ghadhabu zenye kuleta hasara na majuto.

captcha