IQNA

Fikra za Kiislamu

Ni nini maana ya ‘Kumwogopa’ Mwenyezi Mungu?

21:59 - September 05, 2022
Habari ID: 3475738
TEHRAN (IQNA) - Hisia ya woga huja mtu anapokutana na hali ya hatari au ya kutisha. Lakini maandiko ya kidini pia yanazungumzia kuhusu kumuogopa Mwenyezi Mungu. Hofu ina maana gani hapa ilhali Mwenyezi Mungu ameelezwa kuwa ni Mwenye Huruma na Mwenye kurehemu?

Katika Qur’ani Tukufu aya ya 40 ya Sura Al Nazi’at  tunasema hivi: “Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,”. Kulingana na aya hii, mojawapo ya masharti ya wokovu ni kuwa na hofu. Mwenye kuogopa cheo cha Mungu hatashikamana na matamanio yake ya kidunia.

Hofu hii hupatikana pale mwanadamu anapoelewa ukuu wa Mungu Mwenyezi. Uelewa huu utaleta hofu. Kinachowafanya wasomi na wanasayansi wamche Mwenyezi Mungu ni kwa sababu ya kuelewa kwao nafasi yake.

Hii ni sawa na woga aliokuwa nao Musa katika Jabal Muusa: “Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini." (Surah al-A’raf, aya ya 143)

Ufahamu sahihi wa Mwenyezi Mungu hutufanya kumwona akisimamia matendo yetu. Hii inaunda aina ya kujidhibiti kwa wanadamu. Unyenyekevu anaouhisi mtu mbele ya Mwenyezi Mungu ndio unaojumuisha Taqwa, ingawa si kila mtu anaweza kuelewa hili kwa uwazi.

 

Hii ni sehemu ya hotuba ya Ayatullah Seyyed Mostafa Mohaghegh Damad.

captcha