IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Morocco yakamilika

23:10 - September 28, 2022
Habari ID: 3475850
TEHRAN (IQNA) –Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Morocco yalianza Jumanne na kumalizika leo katika mji wa Casablanca magharibi mwa nchi hiyo.

Washindani 60 kutoka nchi za Kiafrika na Asia wanashindana katika kategoria nne za kuhifadhi Qur'ani, usomaji wa Tarteel, Tajweed, na Tafseer (Tafsiri ya Qur'ani).

Shindano hilo litakamilika leo Septemba 28, na washindi watatangazwa Ijumaa.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu ya Morocco.

Wizara hiyo inasema mashindano hayo yamefanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume (SAW) katika mwezi huu wa Rabi al Awwal kama sehemu ya juhudi za wizara hiyo kukuza kuhifadhi Qur'ani, Tajweed na Tafseer.

Morocco ni nchi ya Kiarabu ya Kaskazini mwa Afrika inayopakana na Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania. Uislamu ndiyo dini kuu nchini Morocco, huku asilimia 99 ya watu wa nchi hiyo wakiwa ni Waislamu.

3480652

captcha