Jumuiya ya Morocco ya Kuunga mkono Palestina na Kupinga Uhusiano na Utawala wa Kizayuni wa Israel ilandaa maandamano hayo Jumanne katika kuadhimisha Siku ya Nakba.
Nakba huadhimishwa na Wapalestina kila ifikapo Mei 15 ili kukumbuka kufurushwa mamia kwa maelfu ya Wapalestina katika nyumba na ardhi zao mwaka 1948 baada ya kuasisiwa utawala bandia wa Israel.
Kwa Wapalestina, Nakba ina maana ya tukio chungu na la kusikitisha wakati mababu zao walilazimishwa kutoka katika nyumba na ardhi zao.
Maandamano mengine makubwa yamepangwa kufanyika Jumapili mjini Casablanca nchini Morocco kulaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi dhidi ya Rafah.
Jumuiya ya Morocco ya Kuunga mkono Palestina na Kupinga Uhusiano na Utawala wa Kizayuni imesema katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba serikali ya Rabat lazima ikate mara moja uhusiano wote na utawala huo wa Kizayuni.
Pia imetoa wito kwa vikosi vyote vinavyoiunga mkono Palestina kukaa macho na kuzidisha juhudi katika wakati huu nyeti.
3488348