IQNA

Waislamu Morocco

Zaidi ya Wamorocco milioni 0.4 wanajifunza Qur'ani katika Madrassah

18:23 - November 12, 2023
Habari ID: 3477881
RABAT (IQNA) - Kuna zaidi ya wavulana na wasichana 400,000 wanaohifadhi Qur'ani Tukufu katika Madrassah kote Morocco.

Kulingana na tovuti ya al-Umq al-Arabi, kuna takriban Maktab (Madrassah)12,300 zinazotoa kozi maalumu za Qur'ani katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Aghalabu ya Madrassah hizo ziko misikitini na katika vituo vya vijijini.

Idadi ya wataalamu wa Qur'ani Tukufu  wanaofundisha kwenye Madrassah hizi inazidi 14,000 na wengi wao wamechaguliwa kutoka miongoni mwa maimamu wa misikiti.

Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Wakfu wa Morocco Ahmed Toufiq, ambaye ametoa kauli hiyo akihutubia kikao cha bunge.

Toufiq ameongeza kuwa, dirham milioni 13.2 za Morocco zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wahifadhi Qur'ani wanaojifunza Qur'ani katika Madrassah na pia wasimamizi wa kozi za Qur'ani.

Alisema wizara pia imeanzisha mfululizo wa kanuni za usimamizi wa Madrassah huku akibainisha kuwa hatua hizo zinachukuliwa kwa kuzingatia umuhimu na nafasi ya kihistoria na kiutamaduni ya Maktaba katika kuwafunza wahifadhi Qur'ani.

Morocco ni nchi ya Kiarabu ya Kaskazini mwa Afrika inayopakana na Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania. Uislamu ndiyo dini kuu nchini humo ambapo asilimia 99 hivi ya watu nchini humo ni Waislamu.

4180961

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: morocco qurani tukufu
captcha