IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Nchi 48 za Kiafrika zinahudhuria Mashindano ya Qur'ani ya Morocco

22:00 - September 29, 2024
Habari ID: 3479510
IQNA – Toleo la 5 la Mashindano ya Mohammed VI ya Qur’ani kwa Maulamaa wa Kiafrika yalianza katika mji wa Fes nchini Morocco siku ya Ijumaa.

Wawakilishi kutoka nchi 48 za Kiafrika wanashiriki katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani.

Kuna jumla ya washiriki 118, wakiwemo wanawake 12, wanaoshindana kwa njia ya mtandaoo katka kategoria tatu za kuhifadhi Quran.

Washiriki wanawakilisha matawi ya Wakfu wa Mohammed VI wa African Oulema katika nchi tofauti.

Wajumbe wa jopo la wasuluhishi, wakiwemo wataalamu wa Qur'ani kutoka Morocco na nchi nyingine kadhaa za Afrika, wako katika Fes kutathmini maonyesho ya washindani.

Taasisi hiyo inasema mashindano hayo yanalenga kuimarisha uhusiano wa vijana na Kitabu Kitakatifu na kukuza utamaduni wa kuhifadhi Qur'ani, Tarteel, na usomaji barani Afrika.

Wakfu wa Mohammed VI wa Maulamaa wa Kiafrika, kwa mujibu wa waanzilishi wake, ni taasisi ya kidini ya Kiislamu inayotaka kuzuia misimamo mikali ndani ya Uislamu.

Lengo la msingi ni kuunganisha na kuratibu juhudi za wanatheolojia wa Kiislamu kutoka Morocco na nchi nyingine za Kiafrika ili kuunganisha maadili ya Kiislamu ya uvumilivu na uchunguzi wa kina wa maandiko ya kidini.

Pia inalenga kuwezesha hatua za kiakili, kisayansi na kitamaduni kwa kuwaleta pamoja wanazuoni wa Kiislamu kutoka duniani kote ili kuhimiza uanzishwaji wa vituo vya kidini, kisayansi na kitamaduni na kufanya kazi kuelekea kufufua urithi wa pamoja wa Kiafrika, wa kitamaduni wa Kiislamu.

3490062

Habari zinazohusiana
captcha