IQNA

Fikra za Kiislamu

Jinsi dhambi ndogo zinavyogeuka kuwa kubwa

18:52 - October 11, 2022
Habari ID: 3475914
TEHRAN (IQNA) – Tabia yoyote inayokiuka amri za Mwenyezi Mungu inachukuliwa kuwa dhambi. Kuna aina mbili za dhambi: ndogo na kubwa.

Ingawa dhambi ndogo zitaleta adhabu ndogo, tabia zingine zinaweza kuzigeuza kuwa dhambi kubwa.

Dhambi inaelezwa kuwa ni kufanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu amekataza au kushindwa kufanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu aliamuru. Katika vitabu vilivyoandikwa juu ya maadili, dhambi zimegawanywa katika ndogo na kubwa. Kategoria kama hiyo ina mzizi wa Qur'an:

“Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu.” (An-Nisaa: 31).

Dhambi kubwa ni ile ambayo Qur'ani Tukufu na Hadithi imeitaja kuwa ni kubwa au ambayo wameonya italeta adhabu. Dhambi zingine huchukuliwa kuwa dhambi ndogo.

Ingawa hakuna adhabu kubwa zinazotolwa kwa dhambi ndogo, inaeleweka kutoka kwa aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi kwamba dhambi kama hizo zinaweza kugeuka kuwa kubwa kwa sababu tofauti.

Sababu moja, kwa mfano, ni kusisitiza kufanya dhambi ndogo. Ikiwa mtu atafanya dhambi ndogo na akashindwa kutubu inaweza kuwa dhambi kubwa. Quran inawaambia watu wema:

Na wale ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua. (Surah Al-Imran, Aya ya 135)

Sababu nyingine ni kupuuza dhambi ndogo au kuzidharau. Imam Ali (AS) anasema dhambi mbaya zaidi ni ile ambayo mtenda dhambi huichukulia kwa wepesi.

Mambo mengine yanayoweza kuchangia kufanya dhambi kubwa ni pamoja na kufurahia na kuwa na furaha wakati wa kufanya dhambi, na pia uasi kutokana na dhambi. Quran inasema:

 Basi ama yule aliye zidi ujeuri, Na akakhiari maisha ya dunia, Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! (Surah An-Nazi’at, Aya ya 37-39)

Pia, kufichua dhambi na dhambi zinazotendwa na watu mashuhuri katika jamii kunaweza kuwa sababu ya kuigeuza kuwa dhambi nzito.

Wakati watu wanaojulikana katika jamii wanafanya dhambi, inaweza kuweka msingi wa jamii kupotea na imani ya watu kudhoofika.

captcha