IQNA

Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya yakosolewa kwa kuunga mkono marufuku ya Hijabu

16:09 - October 15, 2022
Habari ID: 3475933
TEHRAN (IQNA) - Mahakama ya juu ya Umoja wa Ulaya (EU) imetoa uamuzi wa kuzuiwa kwa wanawake wenye hijabu kuingia katika maeneo ya kazi, ikidai kuwa marufuku hiyo haimaanishi ubaguzi.

Uamuzi huo umekosolewa na wanaharakati wa haki, huku wengine wakiuita ukiukaji wa "chaguo huru, kujieleza, imani, na uhuru wao wa kimwili (wanawake)."

Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya (CJEU) imetoa uamuzi huo kuhusu kesi ya mwanamke aliyepeleka kampuni kortini kwa kutupilia mbali ombi lake la kazi baada ya kukataa kuvua hijabu ili kutii sera ya kampuni.

Uamuzi huo ni wa hivi punde tu katika msururu wa maamuzi na sheria zenye utata ambazo Waislamu wa Ulaya wanasema zinawabagua.

Kampuni hiyo inasema ina sheria ya kutoegemea upande wowote ambayo inamaanisha hakuna mfanyakazi anayaruhisiwa kuvaa chochote kichwani.

Mwanamke huyo alipeleka kesi kwenye mahakama ya kazi ya Ubelgiji, ambayo ilitaka maoni ya CJEU.

"Kanuni ya ndani ya shughuli inayokataza uvaaji unaoonekana wa ishara za kidini, kifalsafa au kiroho haijumuishi ubaguzi wa moja kwa moja ikiwa inatumika kwa wafanyikazi wote kwa jumla na bila kutofautisha," majaji walisema.

Lakini wanaharakati wa haki na wataalam wa sheria wamekosoa hoja ya mahakama ya "kutopendelea upande wowote".

Kulingana na Human Rights Watch, mawazo ya kutoegemea upande wowote "yamewahi kutumika kuhalalisha marufuku sawa ya sekta ya umma na hii inaeneza mantiki hiyo kwa sekta binafsi, na kufungua mlango wa kuenea kwa ubaguzi wa ajira."

"Mawazo ya mahakama kwamba kuruhusu mavazi ya kidini kunaweza kudhuru uwezo wa biashara wa kufanya kazi kunatokana na mantiki potofu kwamba pingamizi la mteja kwa wafanyikazi wanaovaa mavazi ya kidini linaweza kukandamiza kihalali haki za wafanyikazi," mtafiti mkuu katika Human Rights Watch, Hillary Margolis, aliandika mnamo Juni mwaka jana alipokuwa akijibu maamuzi sawa na hayo kuhusu kesi zilizosikilizwa na mahakama nchini Ujerumani.

Nchini Ujerumani kwa mfano, wanawake wengi wa Kiislamu waliacha kazi zao za ualimu na utumishi wa umma huku mahakama ikiwapa chaguo kamili la kuvua hijabu au kuacha kazi zao.

Kupigwa marufuku kwa mavazi ya kidini na nembo kwa walimu na watumishi wengine wa serikali nchini Ujerumani kulipelekea baadhi ya wanawake Waislamu kuacha kazi ya ualimu.

Nchini Ufaransa, wanawake wanaovaa niqab au burqa, ambayo hufunika uso na mwili kikamilifu, katika nafasi ya umma wanakabiliwa na faini ya euro 150.

Mahakama kuu ya utawala nchini Ufaransa imeidhinisha marufuku iliyopo kwa wanawake wanaovaa burkinis - vazi la kuogelea la kufunika mwili lenye kipande kimoja - katika mabwawa ya kuogelea ya umma.

Uamuzi mwingine wa mahakama ya Ufaransa wa mwaka 2014, wa kupiga marufuku kufunika uso, ulitia moyo polisi kuwatoza faini wanawake 600 wa Kiislamu ndani ya miaka mitatu. Uamuzi huo uliungwa mkono na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu.

Vile vile, wasichana wengi wa Kiislamu waliibiwa haki yao ya elimu wakati Ufaransa ilipopitisha sheria mwaka 2004, inayokataza uvaaji wa hijabu katika shule za serikali.

3480851

captcha