IQNA

Jinai za Israel

Mawaziri wa zamani wa mambo ya nje Ulaya walaani ubaguzi wa rangi wa Israel

7:37 - November 01, 2022
Habari ID: 3476018
TEHRAN (IQNA) - Mawaziri watano wa zamani wa Ulaya wamezitaja sera za utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina kama "kosa la ubaguzi wa rangi".

"Hatuoni njia mbadala ila kukiri kwamba sera na desturi za Israel dhidi ya Wapalestina ni sawa na uhalifu wa ubaguzi wa rangi," walisema katika barua ya wazi iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Ufaransa, Le Monde.

Barua hiyo ilitiwa saini na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Denmark, Mogens Lykketoft; waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Finland, Erkki Sakari Tuomioja; waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Slovenia, Ivo Vajgl; waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ufaransa, Hubert Vedrine na Waziri wa Baraza la Mawaziri wa Uingereza, Sayeeda Warsi.

Mawaziri hao walibainisha ukimya wa jumuiya ya kimataifa ambayo "imeshindwa kuchukua hatua ya sheria " linapokuja suala la mzozo wa Israel na Palestina.

"Wakati ulimwengu unatazama matukio ya kutisha yanayotokea nchini Ukraine, mazungumzo kuhusu uharaka wa kulinda utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria yanatawala mazungumzo ya kisiasa na ya umma. Jumuiya ya kimataifa imejitolea kuunga mkono msimamo wa pande kadhaa na haja ya kuzingatia sheria za kimataifa na kulinda binadamu. Kwa hakika, ndiyo njia pekee ya kusonga mbele katika hali ya kimataifa inayozidi kuwa na mgawanyiko," walisema kwenye barua hiyo.

"Wakati huo huo, tunakumbushwa jinsi jumuiya ya kimataifa mara nyingi imekaa kimya na kushindwa kuchukua hatua mbele ya ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kutokujali kwa ukiukwaji mkubwa katika mazingira mengine," barua hiyo iliongeza.

"Viwango sawa na dhamira ya kulinda raia wa Ukraine na kudai uwajibikaji kwa ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya Russia inapaswa kutumika kimataifa, ikiwa ni pamoja na mzozo wa Israel na Palestina," imesema barua hiyo.

3481042

captcha