IQNA

Iran ina azma mpya ya kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika

19:53 - April 15, 2022
Habari ID: 3475130
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ambapo wamejadili masuala ya kieneo na kimataifa.

Mnamo Alkhamisi, Hossein Amir-Abdollahian amefanya mazungumzo ya simu na  Naledi Pandor Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini. Katika mazugumzo hayo, Amir-Abdollahian amesema bara la Afrika lina umuhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ameongeza kuwa, serikali mpya ya Iran ina azma ya kuimarisha uhusiano na bara hilo, hasa Afrika Kusini.

Amir-Abdollahian ameutahtmini kuwa mzuri uhusiano wa Tehran na Pretoria katika  nyanja mbali mbali. Huku akiashiria kuufanyika kwa mafanikio kikao cha 14 cha tume ya pamoja ya kiuchumi ya nchi mbili amesema Iran iko tayari kwa ajili ya kikao kijacho cha 15 cha tume ya pamoja ya nchi hizi mbili. Aidha amesisitiza kuwa kuna fursa nyingi zilizopo katika uhusiano wa nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo hayo, Naledi Pandor Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusinikwanza amempongeza waziri mwenezake wa Iran kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema Iran ni rafiki wa Afrika Kusini. Aidha  Bi. Pandor amesisitiza kuwa uhusiano wa Iran na Afrika Kusini na umuhimu  mkubwa. Halikadhalika ameipongeza Iran kwa kuunga mkono Afrika Kusini katika taasisi za kimataifa na kuongeza kuwa, Afrika Kusini inaitazama Palestina kama rafiki. Aidha amesema  Cyril Ramaphosa amemualika Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atembelee Afrika Kusini na kuelekeza matumaini yake kkuwa safari tarajiwa ya Rais wa Iran nchini Afrika Kusini itaweka msingi imara wa uhusiano wa nchi mbili.

Amir-Abdollahian amesema Iran na Afrika Kusini zimekuwa zikungana mkono katika taasisiza kimataifa na hivyo amesisitiza kuhusu kuendelea mchakato huo wa ushirikiano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameipongeza Afrika Kusini kwa kuunga mkono kadhia ya Palestina na kusema kuwa, Afrika Kusini kama nchi iliyosuhudia mfumo wa ubaguzi wa rangi au apathaidi na kusema nukta hiyo imeiwezesha kudiriki vyema mfumo wa apathaidi unaotumiwa na Israel dhidi ya Wapalestina.

676614

captcha