"Wakati mashambulio ya makombora dhidi ya Israel yana athari, kukata njia za kiuchumi za Israel kutakuwa na ufanisi zaidi na mkakati huu unapaswa kufuatiliwa kwa muda mrefu," Mirhadi Rahgoshay aliiambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) siku ya Alhamisi.
Maoni hayo yanakuja huku kukiwa na mvutano ulioongezeka katika eneo hilo unaochochewa na uvamizi wa utawala wa Kizayuni Israel kwenye Ukanda wa Gaza na Lebanon na kampeni ya utawala huo ya mauaji dhidi ya viongozi wa muqawama.
"Kuna haja ya Umma na serikali za Kiislamu kuamini kwamba kukata uhusiano wa kiuchumi na Israel ni muhimu," mtaalamu huyo alisema na kuongeza kuwa kushughulikia suala hili sio tu kutapunguza uvamizi wa Israel bali pia kutahakikisha usalama wa eneo na nchi nyingine za Kiislamu.
"Hapo awali, ingeweza kudaiwa kuwa serikali zina ahadi za kisheria na ni tegemezi. Hata hivyo, ikiwa maoni ya umma yataenda katika mwelekeo uliopendekezwa na kuonyesha nia ya kusitisha ushirikiano wa kibiashara na Israel, bila shaka serikali zitalazimika kufuata matakwa ya umma. Mara tu serikali zitakapohusika, zaidi hatua za dhati zitachukuliwa kukata uhusiano wa kiuchumi na Israel, na hatimaye kufanya hali ya uchumi kuwa ngumu zaidi kwa Israel," aliongeza.
Nchi za Kiislamu zinajumuisha chini ya asilimia kumi ya biashara ya nje ya Israel, Rahgoshay alisema, akiongeza kuwa biashara nyingi za utawala wa Israel ziko Ulaya, Marekani na Asia Mashariki. "Hata hivyo, suala muhimu na lenye athari ni kwamba Israel inategemea ushirikiano na nchi jirani na nchi nyingine za Kiislamu kwa ajili ya usafiri. Ikiwa nchi hizi zitakataa ruhusa ya kupita ndege na meli za Israel, bila shaka italeta mazingira magumu kwa utawala huo."
3490223