IQNA

Uislamu nchini Ghana

Msikiti wa Accra kuandaa dua kwa Timu ya Soka Ghana Kabla ya Kombe la Dunia la 2022

17:54 - November 02, 2022
Habari ID: 3476024
TEHRAN (IQNA) – Dua ya Kiislamu imepangwa na Shirikisho la Soka la Ghana (GFA) kwa ajili ya timu ya taifa ya nchi hiyo, inayoitwa Black Stars, kabla ya Kombe la Dunia la 2022 la Qatar.

Dua hiyo imepanga kufanyika Ijumaa, Novemba 4 katika msikiti wa kitaifa huko Accra.

Ibada hiyo itaongozwa na Imamu Mkuu wa Ghana Sheik Osman Nuhu Sharubutu, huku viongozi wa SGFA wakihudhuria.

GFA iliandika: "Kama sehemu ya shughuli zilizopangwa kabla ya Black Stars kushiriki katika Kombe la Dunia la FIFA litakaloandaliwa nchini Qatar, Shirikisho la Soka la Ghana litatembelea msikiti mkuu wa Accra kushika Sala ya Jummah.

"Dua hii maalum itaongozwa na Imamu Mkuu wa Kitaifa, Sheikh Osmanu Nuhu Sharubutu siku ya Ijumaa, Novemba 4, 2022.

"Wajumbe wa baraza kuu, timu ya Ufundi na usimamizi ya Black stars, wafanyakazi wa GFA, makundi mbalimbali ya wafuasi na umma kwa ujumla wote wamealikwa."

Black Stars wanajiandaa kwa Kombe la Dunia, litakaloanza Qatar mnamo Novemba 20.

Ghana wamepangwa Kundi H pamoja na Ureno, Korea Kusini na Uruguay.

Ghana ni nchi iliyoko Afrika Magharibi. Uislamu ni dini ya pili kwa wafuasi wengi nchini humo baada ya Ukristo.

3481093

captcha