IQNA

Sala ya Ijumaa Tehran

Taifa la Iran limesambaratisha njama za maadui

21:04 - December 02, 2022
Habari ID: 3476187
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amezungumzia misimamo ya Iran dhidi ya madola ya kibeberu na kusema kuwa, wananchi wa Iran wamegeuza vitisho vyote vya mabeberu kuwa fursa.

Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqui Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameashiria umuhimu wa takwa na uchamungu na baraka zake nyingi na kusema, Qur’ani Tukufu imetufunza kwamba iwapo taifa litakuwa na uchamungu, Mwenyezi Mungu atatatua matatizo ya maisha yake na kulionesha njia ya kufungua mafundo ya maisha yake. 

Hujjatul Islam wal Muslimin Siddiqui amesema: Taifa la Iran limekabiliwa na fitina na migogoro mikubwa katika kipindi chote cha miaka 43 iliyopita, na limepigana vita vya dunia katika kipindi ambacho karibu nchi zote zilikuwa dhidi yake; lakini halikusalimu amri; lilisimama kidete na kupata ushindi chini ya uongozi wa faqihi mtawala.  

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza kuwa: Taifa la Iran limegeuza vitisho vyote vya mabeberu kuwa fursa, kwa sababu linaamini kuwa taifa zima ni nafsi moja, nguvu moja yenye hekima, na moyo mmoja. 

4103950

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha